WANAWAKE wa Tanzania Red Cross Society (TRCS) wametakiwa kufanya kazi kwa bidii
WANAWAKE wa Tanzania Red Cross Society (TRCS) wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuinua vipato vyao ikiwa ni pamoja na kuendeleza umoja na mshikamano.
Hayo yamesemwa na Rais wa TRCS, David Kihenzile jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani, jana Machi 8, 2022
Amesema, siku hiyo ya wanawake iwe chachu kwa wanawake wa TRCS kuchangamkia fursa mbali mbali mbali ikiwemo ubunifu wa teknolojia ili kujiinua kiuchumi
Amesema wataweka utaratibu wa kimfumo kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele ili waaonyeshe ujuzi wao kupitia nafasi mbalimbali ndani ya shirika hilo
Kihenzile amesema, lengo kuu ni kuimarisha matawi ndani ya taasisi hiyo kwani inaaminika wanawake wanaweza kusukuma maendeleo popote pale duniani.
"Kwa kusema hayo, naunga mkono mapendekezo ya uwepo wa uongozi wa wanawake katika katiba kama ilivyo kwa vijana kuanzia ngazi ya tafa. Nisisitize mjitoe kwa ajili ya chama nakuacha alama za uwekezaji kama walivyoweza kuacha watangulizi wenu. "Amesema
Wakati huo huo wanawake hao wa TRCS wakiongozwa na Katibu wa Taasisi hiyo, Lucia Pande walitembelea wafungwa wanawake katika Gereza la Segerea na kuwapatia mahitaji mbali mbali ikiwemo mafuta ya kupikia, sabun za kufulia, sukari, taulo za kike, Dawa za meno, miswaki, mafuta ya kupaka na sabuni za maji.
Post a Comment