DODOMA WAJIVUNIA KITUO CHA MAFUNZO KWA WAKULIMA WILAYANI KONGWA.
Na Mwandishi wetu - Dodoma.
Mkoa wa Dodoma ni moja ya Mikoa inayokuwa kwa kasi nchini toka kupandishwa hadhi na kuwa jiji kamili na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli.
Katika kuliona hilo Wilayani Kongwa kumejengwa kituo cha mafunzo kwa wakulima na usimamizi wa mazao baada ya mavuno katika eneo la Mtanana Wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari ikiwa ni mwendelezo wa program iliyoandaliwa chini ya Ofisi yake ya kutangaza mafanikio yaliyofanyika ndani ya Mkoa huo katika kipindi cha Awamu ya sita ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
"Sote tunafahamu kuna kitu kinaitwa 'sumukuvu' na kiwanda hiki kitawezesha kuondoa 'Sumukuvu' katika mazao na kuwa na unyevu unaostahili sokoni na hiki ni kituo cha pekee na cha mfano Kwa Afrika Mashariki." amewema Senyamule.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kongwa Dkt Omary Nkullo amesema halimashauri imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya mfuko wa wanawake na vijana na watu wenye ulemavu kwa mujibu wa sheria ili kuwezesha mikopo yenye masharti nafuu na kutoa elimu ya ujasiriamali na biashara ili kuwezesha kuongeza ajira, ujuzi wa kujiajiri, fursa za kipato na kujiamini.
"Fedha iliyotegwa kwa ajili ya mfuko wa wanawake, vijana na wenye ulemavu kutokana na mapato ya ndani imeongezeka kutoka milioni 206,970,900 mwaka 2021/2022 hadi kufikia milioni 294,748,00 mwaka 2022/2023 sawa na ingezeko la asilimia 42.4
Aidha idadi ya vikundi vilivyopatiwa mikopo imeongezeka kutoka vikundi 48 ( wanawake 18, vijana22 na walemavu 8) mwaka 2021/2022 hadi kufikia 98 mwaka 2022/2023 hadi mwezi februari 2023 sawa na ongezeko la asilimia 104.
"Idadi ya wanufaika imeongezeka kutoka 390 ( wanaume 97 na wanawake 293) mwaka 2021 hadi kufikia wanufaika 890 (wanaume 257 na wanawake 676) sawa na ingezeko la asilimiae 128 hadi kufikia mwezi februari 2023" - amesema Mkurugenzi Mtendaji Dkt Omary Nkullo.
Hata hivyo katika bajeti ya 2023/2024 Halimashauri imepanga kutoa mikopo yenye thamani ya milioni 325,199,500 kwa makundi husika

"Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya Miaka hii miwilli imefanya mengi sana,haya niliyoyataja ni sehemu tu ya mengi mazuri yaliyofanyika.Tunampongeza na kumshukuru sana Mhe.Rais"Dkt.Omary Nkullo-Mkurugenzi Mtendaji-Kongwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.
Post a Comment