Header Ads

test

Bank of Africa kuendelea kuwezesha biashara ndogo za kati nchini

 

Bank of Africa Tanzania, imeeleza dhamira yake ya kuendeleza Biashara ndogo na za kati nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kasi na kuleta maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Adam Mihayo, hivi karibuni wakati akieleza ushiriki wa Benki hiyo katika Jukwaa la biashara la Tanzania na nchi za Ulaya (EU-Tanhizania Business Forum) lililomalizika jijini Dar es Salaam.


“Huu ni moja ya mkakati mkuu wa Benki yetu wenye lengo la kuunga mkono dira ya Serikali ya Tanzania katika ajenda ya ujumuishaji katika mfumo rasmi wa kifedha hususani katika makundi ya biashara ndogo na za kati na uwezeshaji wa Wanawake”, amesema.


Mihayo, amesema kuwa Bank of Africa imekuwa na programu ya kuwapatia wafanyakabiashara wadogo na wa kati (SMEs) mafunzo ya uendeshaji biashara zao kwa ufanisi sambamba na kuwapatia mikopo kw ajili ya kukuza biashara zao.


Mkutano wa Jukwaa la Biashara la EU-Tanzania ulilenga kuonyesha fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania na kueleza mikakati ya kufanikisha uwekezaji wa kibiashara kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ulaya na Tanzania.
Bank of Africa, kupitia huduma zake bora na mtandao wake thabiti katika nchi 18 za Afrika imedhamiria kuendelea kufanikisha ushirikishwaji wa kifedha kupitia ubia na ushirikiano.Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Bank of Africa, Nandi Mwiyombella (Kushoto) akisalimiana na waziri wa Nishati, January Makamba wakati alipotembelea banda la maonyesho la benki hiyo kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara la nchi za Ulaya na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Afisa Masoko wa benki hiyo, Beatrice Mirigo (katikati) na Trade Finance Manager,Jesca Mizambwa.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Bank of Africa, Nandi Mwiyombella (Kushoto) akimwelezea jambo Waziri wa Nishati, January Makamba, huduma zinazotolewa na Benki hiyo wakati alipotembelea banda la maonyesho la benki hiyo kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara la nchi za Ulaya na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Bank of Africa,Beatrice Mirigo (katikati) na Trade Finance Manager,Jesca MizambwaBaadhi ya wageni waliotembea banda la maonyesho la Bank of Africa wakipatiwa maelezo ya huduma zinazotolewa na benki kutoka kwa Wafanyakazi wa Benki hiyo.

No comments