Header Ads

test

Baraza la Madiwani Iringa :Daladala zote zirudi kutoa huduma kwa wananchi

 

Na Ashura Godwin, Michuzi TV Iringa 

Halmashauri ya Manispaa ya iringa imewaomba madereva wanaosafirisha abiria  'Daladala' ndani ya Manispaa hiyo kusitisha mgomo na kuendelea na majukumu yao ya kazi.

Ombi hilo limetolewa na Meya wa manispaa ya iringa Ibrahimu Ngwada katika kikao cha baraza la madiwani mapema leo ikiwa ni kutaka wananchi kuendelea kupata huduma huku changamoto zao zikifanyiwa kazi.

Ngwada amesema mgomo wa Daladala huo umetokana na mwingiliano kati ya waenndeshaji wa Pikipiki ya Miguu mitatu Bajaj 

Kwa mujibu wa malalamiko hayo madereva daladala wakilalamikia kulipa tozo mbalimbali za Halmashauri lakini Bajaji zimekua zikiwaingilia katika njia zao jambo ambalo limekua likiwakwamisha biashara zao.

Alisema tayari Halmashauri imekaa vikao zaidi ya 10 kwa ajili ya kusuluhisha jambo hilo ikiwa ni pamoja na kupanga njia ya Daladala pamoja Bajaji.

Amesema baada ya vikao hivyo Bajaj walirudi tena kudai baadhi ya barabara walizopangiwa ni mbovu hivyo Halmashauri kwa kushirikiana na TARULA kuanza marekebisho katika maeneo ambayo walikua wakilalamikia.

Amesema hatua za kutatua changamoto hizo zilifanyika pamoja na kuanza ukarabati katika maeneo ambayo yalikua yakilalamikiwa na utatuzi wa changamoto ya miundombinu ulianza mara moja na bado wanaendelea na uboreshaji wa maeneo yanayo lalamikiwa na madereva wa Bajaj

Aidha amesema Baraza limepewa mamlaka kisheria na hivyo kuvitaka vyombo vingine vinavyoingilia kati utendaji wao wa kazi kufahamu kuwa wao wapo kisheria.

Katika hatua nyingine alimtaka Mkurugenzi pamoja na Afisa Biashara kuhakikisha wanakamata bajaj ambazo zitaendelea kuvunja sheria walizokubaliana nazo katika vikao vyao.
Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwanda akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa kutoa maelekezo ya maazimio ya Baraza hilo.

No comments