Header Ads

test

KATIBU MKUU CCM AISHAURI TIC KUJENGA TABIA YA KUWATEMBELEA WAWEKEZAJI,ATOA MAELEKEZO HAYA KWA TANESCO

 


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV - Ikungi


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo amekishauri Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) kujenga utamaduni wa kuwatembelea wawekezaji waliowasajili ili kuwatatulia changamoto walizokuwa nazo ili kufikia malengo ya Ilani ya CCM katika kuboresha mazingira rafiki kwa wawekezaji

Chongolo ametoa ushauri huo leo Februari 28,2023 alipotembelea Shamba la Kampuni ya Al Fardaws ya kutoka nchini Jordan, lililopo wilayani Ikungi mkoani Singida ambapo ameshangazwa na mwekezaji huyo ambae ameomba huduma ya umeme kwa zaidi ya miezi minne ili awekeze kwenye kilimo cha alizeti.

Kutokana na malalamiko ya kampuni hiyo,Chongolo ametoa mwezi mmoja kwa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kufilkisha miundombinu ya umeme kwa mwekezaji huyo anayetarajia kuwekeza kwenye zao la alizeti.

Awali Mhandisi wa Miundombinu wa Kampuni ya Al Fardaws Edward Nambiza
amesema wanatarajia kuwekeza zaidi ya Sh.bilioni 12.9 katika kilimo cha alizeti ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora za alizeti na kukamua mafuta ya kula.

Kwa upande wake Meneje wa TANESCO Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhandisi Angelo Maskini amesema wanatarajia kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme kufikisha katika eneo la mwekezaji Aprili mwaka huu

Katibu Mkuu Chongolo anaendelea na ziara yake mkoani Singida akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu.





Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Ndugu Miraji Mtaturu (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Ndugu Elibariki Kingu (kulia)mara baada ya kutembelea shamba la mwekezaji la uzalishaji wa mbegu za alizeti la ALFARDAWS lililopo Wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.

No comments