Header Ads

test

KATIBU MKUU DKT. YONAZI APOKELEWA RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU

NA. MWANDISHI WETU- Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amepokelewa rasmi katika Ofisi ya Waziri Mkuu hii leo Februari 28, 2023 Jijini Dodoma na kutoa wito kwa Menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuleta ufanisi.

Dkt. Yonazi amewasihi watumishi hao kufanya kazi kwa juhudi, upendo na Amani ili kuwatumikia wananchi na kuifaya Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea na jukumu lake kubwa la kuratibu shughuli za Serikali kwa matokeo chanya.

Katika hafla hiyo ya mapokezi amewasihi watumishi kuwa wamoja na kufanya kazi kwa weledi zaidi huku akiwashukuru kwa mapokezi mazuri.

“Nimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Sulluhu Hassan kwa kuniteua kuitumikia nafasi hii, ikumbukwe kuwa tuna jukumu kubwa la kuwatumikia wananchi hivyo tufanye kazi kwa juhudi huku tukidumisha ushirikiano,” Alieleza Dkt. Yonazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea ua kutoka kwa Mwandishi Mwendesha Ofisi kutoka Ofisi hiyo Bi. Tusekile Mwakang’ata mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi hiyo, Februari 28, 2023 Jijini Dodoma.Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Stella Mwaiswaga akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo wakati wa haflaya kumpokea kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo Februari 28, 2023Jijini Dodoma.Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi.Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi mara baada ya kuwasili rasmi Ofisini hapo Jijini Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments