Header Ads

test

MASHEHA WATAKIWA KUSIMAMIA VYETI VYA MAZAO

Na Rahma Khamis Maelezo.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka Masheha wa Mkoa huo kusimamia vizuri utoaji wa vyeti vya mazao hasa zao lakarafuu ili wakulima waweze kuuza bizaa zao kwa urahisi zaidi.

Wito huo ameutoa huko Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati katika mkutano wa wakulima na wadau wa karafuu wa kutathmini changamoto zinazowakabili wakati wanapokwenda kuuza karafuu zao katika Shirika la Biashara (ZSTC)

Amesema kuna baadhi ya masheha hawawajibiki ipasavyo katika kutoa vibali kwa wananchi jambo ambalo linawakosesha fursa wakulima kusafirisha bizaa zao kwa ajili ya mauzo ili kujikimu na maisha.

Aidha amefahamisha kuwa Serekali inaendelea kutegemea zao la karafuu katika kuongeza pato la nchi hivyo ipo haja ya kuliendeleza,kulitunza na kulithamini zao hilo kwa maslahi ya Taifa na wnanchi kwa ujumla.

Mkuu huyo ameinasihi Wizara ya Kilimo kuendelea kuvitunza vitalu vya miche ili wakulima wanufaike kwani miche hiyo ni muhimu katika kuendeleza kilimo cha zao hilo.

Akizungumzia suala la uaminifu kwa wakulima Mkuu huyo amesema kuwa kuna baadhi ya wakulma wanajitoa uamnifu kutokana na kuchanganya karafuu na makonyo wakati wa kuuza ili kujiongezea kipato jambo ambalo linapelekea kuondoa haiba ya zao hilo.

Hata hivyo amewashauri wakulima na wananchi kwa ujumla kuwa makini katika kulilinda,kulitunza zao hilo kwani kuna baadhi ya watu wanaweza kuingiza karafuu kutoka nje ya nchi kinyemela na kushusha hadhi ya karafuu ya Zanzibar.

Nae Katibu wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Ali Hilali Vuai amesema kuwa miongoni mwa tathmini ya kazi zao ni kununua karafuu kutoka kwa wakulima ambapo kwa mwaka 2022/23 wamenunua tani 3785.000 zenye thamani ya Sh, 7151661000 za TZ.

Aidha amefahamisha kuwa wamefanikiwa kununua karafuu ambazo hazijachanganywa na makonyo kwa mwaka huu kutokana na kununua mashine za kuchujia na kusema kuwa changamoto inayowakabili ni baadhi ya wakulima kupeleka karafuu ambazo hazijakauka vizuri jambo ambalo sio sahihi.

Kwa upande wao wakulima wa zao hilo wamesema ukosefu wa visima katika maeneo ya mashamba ya mikarafuu imepelekea baadhi ya miti hiyo kufa kutokana na mabadiliko ya Tabianchi.

Aidha wamiomba Wizara ya Kilimo kufanya utafiti wa ardhi ambayo itaweza kuota mikarafuu kwa ili zao hilo lipandwe kwa wingi ZanzibarMkurugenzi Mwezeshaji Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Bakari Haji akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid kufungua Mkutano wa Wadau na Wakulima wa zao la Karafuu ,katika Ukumbi wa Skuli ya Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,tarehe 26 febuari 2023. (PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR)

No comments