MIGIRE AAGIZA TPA KUANZA KUTOA HUDUMA BANDARI YA KWALA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia Sekta ya Uchukuzi
Bw.Gabriel Migire, amewaagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA)
kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali na Binafsi kuhakikisha Bandari
kavu ya Kwala inaanza kazi.
Migire ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Maboresho ya Bandari ya Dar es
salaam ambao umewakutanisha Uongozi wa Usimamizi wa Bandari (TPA), Wizara
na wadau mbalimbali wanaotoa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam.
“Bandari Kavu ya Kwala inatakiwa kuanza kazi haraka ili kupunguza msongamano
wa shehena na Magari makubwa katika Bandari ya Dar es Salaama” alisema Migire.
Aidha, Migire aliongeza kuwa kukamilika kwa Bandari kavu ya Kwala kutasiadia
kupunguza foleni ya magari makubwa katika jiji la Dar es Salaam, hivyo aliitaka kila
taasisi ifanye wajibu wake ili bandari hiyo ianze kufanya kazi.
Kwa upande wake Meneja wa Bandari Kavu ya Kwala, Alexander Ndibalema,
amesema kuwa ujenzi wa Bandari hiyo umefikia asilimia 90 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa Mwezi Machi 2023, pia ujenzi wa Barabara ya Zege ya zaidi ya kilometa kumi na tano kutoka Vigwaza mpaka Bandari kavu ya Kwala imekamika.
Halikadhalika Ndibalema alifafanua kuwa Mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam
itasafirishwa kwa treni mpaka Kwala hivyo anatarajia mizigo kwenda nje ya Tanzania na ndani ya Tanzania yote itachukuliwa katika Bandari hiyo.
Katika hatua nyingine Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho,
amesema kuwa kwa sasa katika bandari ya Dar es Salaam Shehena imeongezeka
kwa zaidi ya asilimia 22 hivyo kutoa wito kwa kila mdau kuhakikisha anawahi
kuhamisha mizigo hasa mizigo ya taasisi za Serikali ambayo inakaa baharini hapo
Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire akizungumza na Wadau wa
Bandari, katika kikao kazi cha uboreshaji wa bandari, kilichofanyika Jijini Dar es
salaam.
unatarajiwa kukamilika Mwezi Machi 2023.
Post a Comment