Halmashauri ya Mji wa Bariadi yapania kumaliza umasikini
KATIKA kuhakikisha umasikini unapungua nchini Halmashauri ya Mji wa Bariadi imemuunga mkono kwa vitendo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza mradi wa kuongeza vipato kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa - TASAF
Halmashauri hii inatekeleza awamu ya nne ya Mradi wa kupunguza umaskini ambapo Jumla ya miradi 15 imetekelezwa ambayo ni miradi 10 ya kuendeleza miundombinu, miradi mitatu ya kutoa ajira za muda na Miradi miwili ya kuongeza kipato cha kaya.
Miradi ya kuendeleza miundombinu inayotekelezwa imegawanyika katika Sekta mbili ambazo ni elimu na afya ambapo kiasi cha Tsh 771,104,382.20 kimetolewa na Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kumi (10) kwa vipindi viwili na kwamba Kila kipindi kilikuwa na miradi mitano.
Kipind cha kwanza kilitolewa kiasi cha Tsh 391,311,075.37 za utekelezaji wa miradi mitano na kipindi cha pili zilitolewa jumla ya fedha Tsh 379,793,306.83 za utekelezaji wa miradi mitano.
Katika sekta ya Elimu miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa madarasa manne na ujenzi wa majengo ya utawala matatu .
Pia katika sekta ya Afya miradi mitatu imetekelezwa ambayo miradi miwili ya ujenzi wa Zahanati na mradi mmoja wa ujenzi wa Nyumba ya Watumishi wa Afya
Kwa upande wa mradi wa kuwaongezea kipato wananchi kumetekelezwa miradi miwili inayohusisha walengwa 134 walio kwenye vikundi 10 kutoka kwenye mitaa 2 kwa kuwagawia kondoo 804 mradi huo umegharimu kiasi cha 44,467,669.78.
Mafaniko ya wazi ya mradi huo ni pamoja na ujenzi wa majengo mbalimbali ambayo mengi yamefikia asilimia 50 , mengine 70 kukamilika mathalan:- wa madarsa mawili Ofisi na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Bunamhala Ufundi uliotengewa kiasi cha 64,990,868. 75 na kutumia kiasi cha 61,819,507 . Ujenzi wa jengo la utawala shule ya sekondari Simiyu ulioyengewa kiasi cha 92,410,714. 29 na kutumika kiacha shilingi 91,806,81 9.
Pia Ujenzi wa Zahanati ya Gisadi uliotengewa kiasi cha shilingi 92,410,714. 29 na uliotumia kiasi cha 88,410,16 9 . Ujenzi wa Zahanati ya Nyangaka uliotengewa kiasi cha 92,410,714. 29 na kutumika kiasi cha 88,734,23 9
Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Zahanati ya Mbiti uliotengewa kiasi cha 49,088,063.75 na kutumia kiasi cha 47,504,239 , Ujenzi wa jengo la utawala shule ya sekondari Matale uliotengewa kiasi cha 92,410,714.29 na kutumia kiasi cha 25,930,204.44 , Ujenzi wa jengo la utawala shule ya sekondari Sanungu uliotengewa 92,410,714.29 uliotumia kiasi cha 25,257,204.44.
Ujenzi wa madarsa mawili , Ofisi na matundu 6 ya vyoo S/m Sima A uliotengewa kiasi cha shilingi 64,990,686.75 na kutumia kiasi cha 17,966,522.44 Ujenzi wa Madarsa 2, ofisi na matundu 6 ya vyoo S/m Isanga C uliotengewa kiasi cha shilingi 64,990,686.75 uliotumia kiasi cha 16,571,522.41.
\ Ujenzi wa Madarsa mawili , ofisi na matundu 6 ya vyoo S/m Yeya uliotengewa kiasi cha shilingi 64,990,686.75 uliotumia kiasi cha16,145,622.44 ,
Miradi iliyokuwa kwenye hatua za awali za ujenzi ni pamoja na Mradi wa Barabara Mwembeni-Nkuli uliotengewa kiasi cha shilingi 66,876,477.50 na kutumia mpaka sasa kiasi cha 1,224,620 , Mradi wa Barabara ya Ng’wang’wali B Mtaa wa Mwagiti uliotengewa kiasi cha shilingi 67,088,531.07 na kutumia kiasi cha shilingi 1,224,620 Mradi wa ujenzi wa kivuko Mwakilalo Mto Masigo uliotengewa kiasi cha shilingi 66,892,857.14.
Pesa zilizotumiaka mpaka sasa ni kiasi cha shilingi 1,224,620 Mradi wa Ufugaji wa Kondoo Mtaa wa Isanga Vikundi vitano ulitengewa kiasi cha 22,220,883.07 na kutumia kiasi cha 1,163,048.18 kilichonunua kondoo 384 pia Mradi wa Ufugaji wa Kondoo Mtaa wa Ng’wakibolo Vikundi vitano litengewa kiasi cha 22,220,883.07 na kutumia kiasi cha 1,163,048.18 kilichonunua kondoo 384.
Jengo la zahanati ya Nyangaka iliyopo katika mtaa wa Nyangaka katika Halmashauri ya mji wa Bariadi lolilojengwa na Tasaf linavyoonekanaWajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya TASAF wakiwa katika moja ya Madarasa mawili yaliyojengwa katika shule ya Msingi Bunamhala, mtaa wa Songambele katika Halmashauri ya mji wa Bariadi.
Post a Comment