Header Ads

test

KATIBU TAWALA SINGIDA AWATAKA TEMESA KUJIENDESHA KIBIASHARA

 

Katibu Tawala  Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga (wa pili kulia) akipata maelezo wakati akikagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Mkoa wa Singida kabla ya kufungua kikao cha wadau na karakana mkoani hapa Machi 29, 2023.

.................................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

KATIBU Tawala  Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga amewataka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) mkoani hapa kujiendesha kibiashara ili kuipunguzia mzigo Serikali ambayo imekuwa ikitoa fedha nyingi kuendesha taasisi hiyo.

Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa ombi hilo leo Machi 29, 2023 wakati akifungua kikao cha wadau na karakana ya Mkoa wa Singida ambacho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Matengenezo na Huduma za Ufundi Temesa Makao Makuu Dodoma, Mhandisi Hassan Koronda.

“Tengenezeni magari kwa ubora na weledi punguzeti gharama za uendeshaji ili muisaidie Serikali na mkimbiliwe na wateja” alisema Mganga.

Aidha, Mganga aliwataka TEMESA kutumia fursa waliyonayo kutoka nje kujitangaza ili wafahamike badala ya kukaa tu ofisini na akaishauri kuanza kutumia TEHAMA kwa ajili ya kupata mrejesho kutoka kwa wateja wao kupitia ujumbe mfupi.

Mganga alihimiza TEMESA kutoa mafunzo kwa madereva  ya uendeshaji wa magari ili wajue mbinu ya kuyatunza ukizingatia kuwa ni wadau wao na akaomba waanzishe kitengo cha uoshaji wa magari ili iwe motisha kwa wateja wanaowapelekea vyombo vyao vya moto.

Akizungumzia madeni yanayodaiwa na TEMESA aliomba apewe orodha ya wadaiwa wote zikiwepo Taasisi za Serikali ili aweze kuonana na wahusika waanze kulipa madeni hayo kwa awamu.

“Serikali inayomatarajio makubwa kuona mnafanya kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya sheria za utumishi wa umma na kanuni zake kwa kutumia Taaluma zenu kutunza mali za umma hasa magari na miundombinu ya umeme kwani nagharimu fedha nyingi,” alisema Mganga.

Mkurugenzi wa Matengenezo na Huduma za Ufundi , Mhandisi Hassan Koronda alisema Serikali imekua ikitenga fedha kila mwaka na mwaka huu wa fedha wa fedha kiasi cha Sh.Bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa karakara kumi na mbili katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Singida ambao ujenzi wake wa awamu ya kwanza tayari umekamilika.

Aidha, Koronda alisema Serikali imetoa kiasi cha fedha Sh.509.8 Milioni kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa kwa upande wa umeme, ICT na mitambokwa karakana za mikoa yote Tanzania kwa lngo la uboreshaji utendaji wa kazi.

Mkuu wa Magari,  TEMESA Mkoa wa Singida, Erasto Cheza akitoa taarifa ya mikakati ya utendaji wa kazi alisema wameyaondoa malalamiko yaaaaaliyokuwepo awali kwa kuyatambua na kuandaa mikakati ya kuyamaliza kabisa kwa kushirikiana na wadau wao, mabadiliko ya tabia, matendo na mwenendo kwa kupata elimu ya kuendana na mahitaji ya wateja.

No comments