MAKAMU MWENYEKITI UWT AIHIMIZA USHIRIKIANO KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA
Na Mwandishi Wetu Michuzi TV
Ametoa kauli hiyo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati wa Kongamano la Wanawake katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayofanyika kila Machi 8 ya kila mwaka ,hivyo amesema ili kukabiliana a ukatili wa kijinsia kwenye jamii,ni vema kukawa na ushirikiano wa kuibua matukio hayo ili wahusika wachukuliwe hatua.
"Wafichaji wakubwa wa taarifa hizi ni wakina mama kwa sababu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia ni ndugu wakaribu ,unaweza kukuta anayefanya wakati mwingine ni Mjomba, baba wa kufikia, kaka au wageni wanaokuja nyumbani.Hivyo mama akisema anahisi ndoa itavunjika au atavunja udugu."
Makamu Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa iko haja ya sheria kuongezewa ukali kwa wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji na ikiwezekana wanaofanya hivyo wahasiwe na hivyo kukomesha kabisa vitendo hivyo.
"Awali nilikuwa naibu waziri wa wizara hii na tumefanya mambo mengi ikiwemo kuunda vikundi vya ufugaji, na uvuvi kwa kuwapatia kinamama majokofu ya kuifadhia samaki wasiharibike pamoja na kutoa mbegu bora ya ng'ombe wa kisasa ili kuwawezesha kiuchumi."


Post a Comment