SERIKALI YAPOKEA SHEHENA YA DAWA KUTOKA R4D
Na WAF- DSM.
Serikali inapokea yapokea shehena ya mwisho ya dawa aina ya “Amoxicillin Dispersible Tablets” zilizotolewa kwa msaada na shirika lisilo la Kiserikali la Result for Development (R4D) katika kipindi cha mwaka 2017-2023.Shehena hiyo imepokelewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya katika ofisi za MSD Jijini Dar es Salaam.
Akipokea Shehena hizo, Dkt. Mollel amesema, kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa hali ya upatikanaji wa Dawa hizi katika vituo vya kutolea huduma imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia zaidi ya asilimia 90 mwaka 2022.
Ameendelea kusema kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa unaotelewa na R4D ambapo katika kipindi cha mwaka 2017-2023 jumla ya bidhaa zilizopokelewa katika kipindi hicho ni vidonge milioni 212 vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania Billion 8.8, ambapo takribani watoto milioni 14 wamenufaika.
Aidha, Dkt. Mollel amesema, upatikanaji wa dawa hii umechangia kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 67/1000 (TDHS) 2015/16 hadi 43/1000 mwaka TDHS (2022).
Pia, amesema, wakati msaada huu unafikia ukomo mwezi huu Machi 2023, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeweka mpango wa ununuzi wa dawa hii kupitia Bohari ya Dawa ili wananchi waendelee kunufaika na huduma hii.
Post a Comment