Header Ads

test

WATANZANIA WAASWA KUJITOLEA KWA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

 

APRIL. 23.2023 AHMAD NANDONDE KISARAWE PWANI.

KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kisarawe  NASRI MKALIPA ametoa wito kwa vijana kujijengea utamaduni wa kutembelea vituo vinavyowalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu sanjari na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo hatua itakayowasaidia kufikia malengo yao.

MKALIPA ametoa wito huo baada ya kuungana na wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule ya Sekondari KIMANI katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha KISARAWE ORPHANAGE CENTER kilichopo Kata ya Kisarawe.

katibu huyo amesema kuwa endapo vijana wengi wakijenga tabia ya kuwatembelea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu itakuwa fursa kwao kujifunza zaidi na kuwa na moyo wa huruma katika kuwasaidia kuliko kupoteza fedha nyingi katika starehe ambazo ni za muda mfupi tofauti na kuwekeza katika watu.

Aidha MKALIPA ameitaka jamii kujitolea kwa dhati kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji, ikiwa pamoja na kuwatembelea ili kujenga upendo kwa makundi maalumu yenye uhitaji kwa lengo la kupunguza changamoto zinazoyakabili makundi hayo.


No comments