Header Ads

test

MANISPAA SINGIDA YANUNUA MAGARI YA KUZOLEA TAKA

 


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jeshi Lupembe (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na madereva wa Manispaa hiyo mbele ya magari ya kuzolea takataka  yaliyonunuliwa na Manispaa hiyo yenye thamani ya Sh. Milioni 200. 

Thobias Mwanakatwe na Dotto Mwaibale, Singida  

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida imenunua magari mawili ya kuzolea taka yaliyogharimu zaidi ya Sh.Milioni 200 ikiwa ni mkakati wa manispaa hiyo kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jeshi Lupembe, alisema magari hayo ambayo yatazinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba, yamenunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani zilizotengwa katika  bajeti ya 2022/2023.

Alisema katika mapato hayo ya fedha za ndani Manispaa inajenga kituo cha Afya Mtipa kwai Sh.milioni 500, kujenga machinjio ya kisasa Sh.Milioni 120, kujenga jengo la utawala ghorofa tatu eneo la karakana fedha kutoka serikali kuu Sh. bilioni moja kwa awamu ya kwanza na Sh. milioni 31 zimetumika kulipa fidia ya dampo Mwankoko.

Lupembe amewaomba wananchi wa Manispaa ya Singida kutoa ushirikiano kwa kuhifadhi taka taka kandokando ya barabara ili magari hayo yatakapopita yaweze kuzichukua.

"Jukumu ya kuuweka mji katika hali ya usafi ni la wananchi wote na sio la watendaji wa Manispaa, haipendezi kuona mtu anatupa taka ovyo barabarani, sasa tumenunua haya magari tuyatumie ili kuuweka mji wetu kwenye usafi," alisema Lupembe.

Aidha, Lupembe alihimiza wananchi kufanya usafi maeneo ya kaya zao na kupanda miti minne kila kaya, kulipa ada ya taka sh 2000 na wafanyabiashara sh 5000 kwa mwezi ili kudumisha usafi wa mji na kuboresha mazingira .

Katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Manispaa ya Singida ilitangaza kutumia zaidi ya Sh Milioni 701.6  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ununuzi wa magari ya kuzolea taka fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa Singida, Serukamba aliwataka Wananchi wa Manispaa ya Singida  kuhifadhi takataka wanazo zalisha majumbani mwao badala ya kuzitupa barabarani au kuzipeleka kwenye majalala huku Halmashauri ya Manispaa hiyo ikiagizwa kuweka utaratibu wa kupita kila kaya kukusanya taka hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jeshi Lupembe,

No comments