MFALME KWENYE UFALME WAKE KURINDIMA TENA APRIL 22 MJI KASORO BAHARI.
MWAANDAJI wa Mapambano ya Ngumi za Kulipwa nchini Peaktime wazindua rasmi pambano la "Mfalme kwenye ufalme wake'' linalotarajiwa kufanyika Aprili 22,2023 Ukumbi wa Tanzanite Mji Kasoro Bahari Morogoro.
Akizungumza na Wanahabari, wadau wa ngumi Morogoro mara baada ya kumaliza zoezi la kupata futari pamoja na watoto yatima Mratibu wa matukio kutoka 'Peaktime ' Bakari Khatib amesema Kampuni hiyo imekuwa ni ratiba ya kila mwaka unapoanza kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya Kuonesha vipaji vyao vichanga ambavyo havijapewa nafasi kuonekana.
Hata hivyo Khatib amesema pambano hilo litakuwa na burudani kedekede kwani kutakuwa na visasi ambavyo mabondia wamekuwa wakitambiana na kubaki na utata nani bingwa .
Aidha,amesema Pambano kubwa (Maincard) litabebwa na Mkali Twaha Kiduku dhidi ya mpinzani wake Lago kiziria kutoka Georgia .
Mabondia wengine watakaosindikiza pambano hilo ni pamoja na Habibu pengo atakaevaana na hasimu wake Said mkola,Pascal monyata dhidi ya Ahmed Pelembela nae Mchapeni akimkanda Mgogo.
Kwa upande wake Bondia Twaha Kiduku amesema amejiandaa vizuri kuelekea pambano hilo na anatarajia Kushinda kwa kishindo na kuwaomba wakazi wa Morogoro na Mikoa mengine ya karibu kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hiyo.

Post a Comment