MRADI WA ESCHOOLTZ KUNUFAISHA SHULE 30 MKOANI PWANI NDANI YA MIEZI SITA-MWL HAMIS
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MRADI wa EschoolTz, unaolenga kutatua changamoto ya utoro na udanganyifu katika shule za Msingi na Sekondari unatarajia kufikia shule 30 ,kwa kipindi cha miezi sita Mkoani Pwani ,kwa gharama ya sh.milioni 38.
Akitoa ufafanuzi katika uzinduzi na kukabidhi vifaa vya mradi, uliofanyika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani, Mwalimu wa shule ya Sekondari Pichandege, Hamis Saidi ambae ndio mbunifu wa mradi,alieleza mradi huu unaanza mwezi april hadi September mwaka huu kwenye Halmashauri ya Mafia na Kibaha Mjini.
Alisema ,kwa Halmashauri ya Mafia Mradi utafikia shule 12 kati ya hizo sita za Msingi na sita za Sekondari na Halmashauri ya Kibaha Mjini, utafikia shule 18 ikiwemo Tisa za Msingi na Tisa Sekondari.
Hamis alielezea, EschoolTz ni mfumo wa komputa unaosaidia Tawala ya shule za Msingi na Sekondari katika Tanzania utawala wa mawasiliano ni WA kuongeza ufanisi.
"Ni ubunifu nilioubuni Mimi mwenyewe na kuibuliwa na Serikali kupitia mashindano ya Kimataifa ya Sayansi na Teknolojia na ubunifu"alisema Hamis.
Mbunifu huyo alitaja malengo ya EschoolTz kuwa ni, kutatua changamoto ya utoro, udanganyifu kupunguza gharama za muda na fedha na kuongeza idadi ya wahitimu katika shule za Msingi wanaomudu stadi za KKK, ujuzi na maarifa yenye kuleta ushindani kwenye soko la ajira.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech ),,dkt. Prosper Masawe alisema Costech imegharamia mradi huo kiasi cha sh.milioni 38.
Alieleza , kufuatia changamoto kubwa ya mawasiliano , mfumo wa Eschool utarahisisha mawasiliano kuanzia ngazi ya Mwalimu na Mwanafunzi ,utadhibiti udanganyifu .
Nae Meneja wa DTBI Elia Kichaga alieleza, DTBI inashughulika kusaidia na ubunifu wa vijana wa kitanzania,lengo ni kuhakikisha bunifu hizo zinainuka kiuchumi ndani ya jamii zetu.
Alisema , ubunifu wa Hamis utasaidia si tu shule bali Taifa kijumla kuleta matokeo chanya.
" Dunia inapokwenda na lengo la mfumo vinakwenda Sambamba kwani mfumo huu unatengeneza uwajibikaji na uwazi kuanzia kwa mwanafunzi,*Ni Lazima tutengeneze demokrasia yetu ya uwajibikaji na upatikanaji wa taarifa kirahisi,na kwa kupitia mfumo huu itasaidia kwa kiasi kikubwa"alibainisha Elia.

.jpg)
Post a Comment