TAASISI YA ISHIK YAKABIDHI MADARASA MAWILI YA MILIONI 33/- SHULE YA MSINGI MIKOCHENI A
Na Ashrack Miraji
TAASISI ya Ishik Medical Foundation ambayo inamilikiwa na Shule ya Feza nchini imezindua majengo ya madarasa mawili ambayo yamegharimu Sh.milioni 33 na kukabidhiwa kwa Shule ya Msingi Mikocheni A.Hatua ya taasisi hiyo kujenga madarasa hayo na kukabidhi kwenye shule hiyo ni sehemu ya jitihada zao za kuendeleza juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Samiha Suluhu Hassani za kujenga madarasa kwenye shule za Msingi na sekondari ili wanafunzi wapate elimu bora,
Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa majengo hayo ya madarasa, Mkurugezi wa Shule za Feza Tanzania Ibrahim Yunus amesema Taasisi hipo imekuwa karibu na Serikali katika kusaidia shughuli za kijamii hasa katika jitahada za kumuunga mkono Rais Samia ambaye anafanya kazi kubwa katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake Diwani wa Mikocheni A Hussein Zenzel ametoa shukuru kwa niaba ya Serikali kwa taasisi hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo na Serikali itaendelea kushirikiana kwa pamoja na wadau hao ili kuleta maendeleo katika jamii na kuzitaka taasisi nyingine ambazo siyo za kserikali kuendelea kutoa huduma za kijamii katika nchi yetu.
Post a Comment