TANZANIA YASHIRIKI UFUNGUZI MKUTANO MKUU WA AFYA WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI 'WHO' GENEVA USWISSI
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Nassor Mazrui, Waziri wa Afya Zanzibar (katikati) wakishiriki matembezi yaliyotangulia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 76 wa Afya yaliyokuwa na ujumbe “Walk the talk; health for All challenge”, yaliyofanyika jijini Geneva, Uswiss tarehe 21 Mei, 2023. Wengine katika picha ni Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Seriklali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Geneva(kulia) na kutoka kushoto ni Dkt. Seif Shekalaghe, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (wa pili toka kushoto).
Mhe. Nassor Mazrui, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Seriklali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Geneva wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wengine baada ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 76 wa Afya, Geneva, Uswissi tarehe 21 Mei, 2023.
Mganga Mkuu wa Seriklali, Prof. Tumaini Nagu akitoa mchango wa Tanzania katika mkutano ulioratibiwa na Jumuiya ya Madola ikiwa ni sehemu ya Mkutano mkuu wa 76 wa Afya, uliofanyika tarehe 21 Mei, 2023, Geneva, Uswiss. Katika mkutano huo Prof. Nagu alieleza mkutano hatua mbalilmabli zilizotumika Tanzania katika kudhibiti maambukizi ya majanga ya UVIKO 19 na ugonjwa wa Marburg uliotokea mkoani Kagera na akasisitiza umuhimu wa nchi Wanachama Jumuiya ya Madola kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe akichangia mada katika mkutano Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 21 Mei, 2023, Geneva, Uswiss kabla ya kuanza kwa Mkutano mkuu wa 76 wa Afya. Dhumuni la mkutano ni Wanachama wa AU kuweka msimamo wa pamoja wa kuzuia, kujiandaana na kukabiliana na maambukizi ya UVIKO 19. Dkt. Shekalaghe alikichangia mada hiyo alieleza umuhimu wa kujenga viwanda vya ndani ili kuzalisha dawa na vifaa tiba katika nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika. Vile vile alilsistiza kufanyika mapitio ya sheria za Kimataifa zinazohusika na masuala ya usawa katika biashara.Mhe. Nassor Mazrui, Waziri wa Afya Zanzibar akiongoza ujumbe wa Tanzania wakishiriki kwenye mkutano wa kikao cha kundi la Afrika cha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 76 wa Afya unaofanyika Geneva, Uswissi tarehe 21hadi 30 Mei, 2023. Katika kikao hiki kundi la nchi za Afrika hukutana kabla kwa maandalizi na kukubaliana katika masuala yatakayojadiliwa na mkutano mkuu ili kuwa na sauti ya pamoja
Post a Comment