JUNI.19.2023 AHMAD NANDONDE KIBAHA. SCRIPT.
TAASISI ya kumbukumbu ya Mwalimu Julias Nyerere yaungwa mkono kuhamasisha watu kujitolea damu kusaidia wagonjwa ambapo chupa 35 zimepatikana.
Hayo yalisemwa Mlandizi na Yahaya Mbungulume ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha baada ya zoezi la uchangiaji damu lililofanywa kwa pamoja na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julias Nyerere kwa kushirikiana na Taasisi ya Chawa wa Mama Kibaha Vijijini na watu binafsi wametakiwa kujitokeza kuchangia damu ili kunusuru wagonjwa wanaohitaji damu kwani ni muhimu katika kuokoa maisha ya watu.
Mbungulume alisema kuwa damu huwa haitoshi na inahitajika muda wote kwa ajili ya wagonjwa wakiwemo wajawazito, wagonjwa wa ajali na wagonjwa wa kawaida wanaohudumiwa kwenye Hospitali mbalimbali nchini.
Alisema damu ni sehemu muhimu ya tiba kwa wagonjwa amewataka Watanzania kujitolea kuchangia damu.

Kwa upande wake katibu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani Omary Pumzi alisema kuwa waliamua kujitolea damu baada ya kupita kwenye Hospitali na kuona jinsi gani kuna uhitaji mkubwa wa damu.
Pumzi alisema kuwa Taasisi hiyo imeendelea kutekeleza malengo ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya kukabilana na adui wa maendeleo ambao ni maradhi ujinga na umaskini hivyo afya ni moja ya malengo kwama yalivyo kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Akiongoza zoezi la uchangiaji damu Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Mwalimu Taifa Neema Mkwachu alisema wanamuunga mkono Mwasisi wa Taifa kwa vitendo kwa kushiriki moja kwa moja.
Akielezea mafanikio ya zoezi la uchangiaji damu mratibu wa huduma za maabara Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Nabwike Mwairinga alisema kuwa wamepata uniti 32 kwenye zoezi hilo ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye benki ya damu ambapo wanahitaji uniti 40 kwa kila mwezi.

Post a Comment