Header Ads

test

MALKIA WA NGUVU ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amemtunuku tuzo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu kitaalam Himofilia Dk. Stella  Rwezaula kutokana na mchango wake katika kuwahudumia wagonjwa wa damu hasa wenye ugongwa wa selimundu (Sickle cell).

Dk.Stella ambaye pia ni Malkia wa Nguvu Clouds Media Sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii amewahi kupata tuzo mbalimbali za ndani na kimataifa kwa kutoa mchango mkubwa katika kuanzisha kliniki za magonjwa ya Damu katika hospital mbalimbali hapa nchini ikiwemo Muhimbili anakofanyia kazi hata sasa.

Dk.Stella anapata tuzo hiyo ikiwa ni katika kusherehekea siku ya siko seli Kimataifa huku akiwa na sifa nyingine ya kuwa Daktari wa kwanza mwanamke nchini kupandikiza wagonjwa uroto.


 

No comments