SAKATA KUVUNJWA KWA BAA YA BIG MOUNT LAFIKA KWA WAZIRI MAMBO YA NDANI, KUFUATILIA JALADA LA KESI
Na Mwandishi Wetu
SAKATA la Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam (ZCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faustine Mafwele kuzuia askari polisi wa kituo cha Stakishari kukamata watuhumiwa wanaohusika katika jalada namba STK/IR/11978/2022, limetua mezani kwa
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema amepokea amepokea malalamiko ya mmoja wa askari wa Kituo cha Polisi Stakishari kuzuia askari wenzake kukamata watuhumiwa wanaohusika katika jalada namba STK/IR/1978/2022.
Katika malalamiko hayo yaliyotua mezani kwa Waziri Masauni yanahusu askari huyo kudaiwa kuzuia askari wenzake kufanya upelelezi wa jalada lililokuwa mezani kwao katika kituo hicho kwa maslahi yake binafsi kwa kushirikiana na mtuhumiwa anayetajwa kuwa ni bilionea Wilson Kiguha Chacha, hivyo ameahidi kulifanyia kazi suala hilo haraka iwezekanavyo ili haki itendeke.
“Nimepokea malalamiko ya askari wangu akilalamikiwa kukwamisha upelelezi kwa lengo la kuhakikisha jalada hilo pamoja na watuhumiwa hawafikishwi Mahakamani, ikibainika tuhuma hizo ni za kweli hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya askari huyo mara moja.
"Tuhuma hizi ni nzito kwa askari wangu hivyo nipeni muda nilifatilie jambo hili kwa kina,"amesema Waziri Masauni baada ya Mwandishi wa habari kutaka kufahamu kama amepokea malalamiko ya askari wa kituo hicho kudaiwa kuzuia mwenendo sakata hilo.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa pale wanapoona kunaviashiria vya kuminywa kwa haki zao na askari polisi ili hatua kali zichukuliwe kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo huku akisisitiza askari wote kufanya kazi kwa weledi kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Askari huyo anatuhumiwa kunyakua jalada na kutokomea nalo lenye kesi ya uvunjaji na wizi wa mali katika Bar ya Big Mountain, hivyo kukwamisha upelelezi ambapo hivi sasa ni zaidi ya miezi sita (6).
Jalada hilo namba STK/IR/11978/2022 lililokuwa likiwahusu wafanyakazi wa Kampuni ya Wikicha Estate Development Agency inayomilikiwa na mfanyabiashara Wilson Chacha inayo miliki na kusimamia shughuli zote zinazofanywa kwenye kiwanja namba 48766 kilichopo Ukonga Banana jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa askari huyo aliyetajwa kwa jina la ACP Faustine Mafwele anatuhumiwa kutumia mamlaka yake kupiga marufuku askari wote wa kituo hicho kukamata muhusika yeyote aliyehusika kwenye tukio la uvunjaji wa bar hiyo.
Hata hivyo Mafwele alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo hakukubali wala kukataa na badala yake alisema yeye si msemaji hivyo atafutwe kiongozi wake.
Aidha imedaiwa mwingine anayeratibu kukwamisha upelelezi ni Kamisha Mstaafu wa jeshi hilo Linus Sinzumwa ambaye pia ni mpangaji anayendesha shughuli zake za kibiashara kwenye moja ya maduka yaliopo kwenye eneo hilo.
Hata hivyo alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi kuhusu tuhuma hizo alikanusha vikali na kueleza yeye hajawahi kufanya hivyo na kama wameshindwa kufanya upelelezi ni uzembe wao.
“Siwezi kuwazuia Polisi kufanya kazi yao, kama wameshindwa kufanya upelelezi wa jambo hilo hao ni wazembe wanastahili kuwajibishwa, ”amesema (CP) Mstaafu Sinzumwa.
Habari zisizo na chembe ya shaka kutoka kwa mmoja wa wanafamilia zinadai kuwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo mzee Wilson Kiguha Chacha sasa ana haha huku na kule kuhakikisha jinai hiyo haifikishwi Mahakamani kwa lengo la kuficha uovu huo.
Mwanafamilia huyo ambaye jina (tunalo) amesema kuwa hivi sasa Mzee Chacha amekuwa akifanya mawasiliano na viongozi mbalimbali na wakati mwingine viongozi hao hufika nyumbani kwa ajili ya mazungumzo akiwataka wamsaidie jambo hilo lisifikishwe Mahakamani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mzee Wilson Chacha amesema hajakutana wala kuzungumza na kiongozi yeyote mkubwa wa Jeshi la Polisi wala taasisi yoyote ya Serikali huku akitaka kufahamu mwanafamilia aliyetoa madai hayo.
Alipotafutwa mmiliki wa bar ya Big Mountain alielekeza atafutwe wakili wake Wakili Frank Chundu ambaye amesema wao wanasubili maamuzi ya Polisi kupeleka kesi mahakamani.
Waliokamatwa na kuhojiwa na Polisi hadi sasa ni Godfrey Chacha ,Joseph Nyagare, Michael Julius Chacha, Amosi Chacha, Elizabeth Kiguha, Ramadhani Salehe (Sheta), Amiri Kaswe(White) na Josephat Mlaki ambao ndio wanamiliki wa mtambo uliotumika kuvunja.
Wengine ni Ally Mbulu na Jafari Mbulu ambao ni wamiliki wa kampuni ya udalali inayoitwa Mak Auctioneers Company LTD waliopewa kandarasi ya kuvunja bar hiyo na wakili wa Mzee huyo Juvenalis Motete.
Post a Comment