Header Ads

test

WANAFUNZI WANAOFANYA TAFITI ZA KISAYANSI WASHAURIWA KUENDANA NA KASI YA UKUAJI TEKNOLOJIA VIWANDANI

Na Mwandishi Wetu

MWANZILISHI Mwenza wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST)  Dr. Kamugisha ametoa rai kwa wanafunzi wanaofanya tafiti zenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto kuhakikisha wanatumia teknolojia ya hali ya juu ikiwemo kutumia akili bandia.

Kwa mujibu wa Kamugisha amesisitiza kutumika kwa teknolojia ya nne ya mapinduzi ya viwanda yatakayowezesha kuongeza umahiri na hivyo kulinda nafasi zao katika ulimwengu unaonda kwa kasi kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa.

Kamugisha ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Maonyesho ya Sayansi na teknolojia kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Ambapo pamoja na mambo mengin ameelezea uwepo wa muamko mkubwa wa wanafunzi kujihusisha na tafiti za kisayansi na ugunduzi mbalimbali nchini

Ameongeza hali hiyo imefanya kwa mwaka 2023 wanafunzi takribani 979 wamewasilisha maombi ambapo kati yao tafiti 361 zimepatiwa usaidizi huku akibainisha baadhi ya kazi za kisayasi zitakazoonyeshwa kwenye maonyesho ya mwaka huu zimejikita katika masuala ya utunzaji wa mazao ya kilimo.

Pia utunzaji wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali maji, uzalishaji wa umeme hivyo kuwataka wadau na jamii kwa ujumla kuwaunga mkono wanafunzi hao.

Awali Ofisa mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Caren Rowland amesema taasisi hiyo imeendelea kuboresha program zinazolenga kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.

Amesema lengo ni kuwawezesha kuendana na sera ya nchi katika kuleta maendeleo endelevu kupitia uboreshwaji wa miundombinu m ya elimu na uwezeshaji na hatimaye kutengeneza kizazi cha wasomi na wabobezi.

Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania (YST) Dr Gozibert Kamugisha (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo  jijini Dar es Salaam.
Waandishi  wa habari wakimsikiza Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Young Scientists Tanzania (YST) Dr. Gozibert Kamugisha.


No comments