Airtel Money yaendelea kuboresha maisha ya watanzania
Na mwandishi wetu.
WATEJA wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, wametakiwa kuendelea kushiriki katika promosheni ya Upige Mwingi na Airel inayoendelea kwa muda wa miezi mitatu, kwa kutumia huduma za Airtel Money kwani zawadi bado zipo nyingi na za kutosha
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Bi. Adriana Lyamba jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni hiyo na kuwataka wateja wa kampuni hiyo kuendelea kufanya miamala mingi ili kujiweka katika nafasi nzuri za kujishindia zawadi.
“Sisi kwetu mteja ni wa thamani sana na ndio maana kila siku tumekuwa tukiwaletea promosheni mbalimbali ili waendelee kufurahia huduma zetu bora zinazotolewa na Airtel, kupitia ‘Upige Mwingi na Airtel’ ambayo zawadi zenye thamani ya takribani milioni 250 zitatolewa, kila mteja anapotumia huduma yoyote ya airtel anaweza kushinda zawadi.
“Wateja wetu waendelee kuupiga mwingi, zawadi zipo nyingi, kuanzia pesa taslimu, laki moja, milioni moja, pikipiki, bajaji, jokofu, televisheni, muda wa maongezi, bando za intaneti na mwisho zawadi kubwa ya pesa taslimu kiasi cha shs milioni 50”, alisema Bi. Adriana.
Akipokea zawadi ya smart televisheni aina ya Samsung inchi 50, mkazi wa Dar es Salaam, Hussein Hussein alisema hakutarajia kushinda zawadi hiyo na kuwataka wateja wengine kuendelea kuchangamkia promosheni ili washinde kama yeye, huku Sabrina Joseph aliyeshinda zawadi ya Jokofu yeye alisema zawadi hiyo inampa ari ya kuendelea kuupiga mwingi ili aendelee kushinda zawadi zaidi ikiwemo zawadi kubwa ya shs milioni 50.
Katika hafla hiyo pia Airtel kwa kushirikiana na Benki ya Letshego Faidika ilikabidhi zawadi ya bajaji kwa mshindi wa promosheni yao ya ‘Vimba na Timiza Akiba Ushinde’ ambapo mkazi wa Dar es Salaam, Peres Masige aliondoka na bajaji hiyo yenye thamani ya shs milioni 7.5.
Akizungumza, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Letshego, Asupya Bussi alisema ili kushinda zawadi mteja wa Airtel Money alitakiwa kujiwekea akiba katika huduma ya Timiza inayoendeshwa kwa ushirikiano wa benki hiyo na Airtel.
“Promosheni ya Vimba na Timiza Akiba Ushinde lengo lake kuu ilikuwa ni kuwafanya wateja wa Airtel na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ili kushinda zawadi na pia kujimarisha kiuchumi”,alisema Bwana Bussi.
Mkurugenzi wa kitengo cha Huduma kwa Wateja Kampuni ya Airtel Adriana Lyamba (wa pili kushoto), kikabidhi zawadi ya bajaji kwa mkazi wa Dar es Saalam, Bwana Peres Masige aliyeibuka kidedea katika promosheni ya Vimba na Timiza Akiba Ushinde jijini Dar es Salaam leo. Promosheni hiyo iliyoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Letshego, mshindi alitakiwa kuweka akiba kwa kutumia huduma ya Timiza inayopatikana kwa watumiaji wa Airtel Money. Kulia ni binti ya mshindi huyo, Mary Mbasha
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika, Bwana Asupya Bussi (katikati), akikata utepe kuashiriria makabidhiano ya bajaji kwa mshindi wa promosheni ya 'Vimba na Timiza Ushinde' mkazi wa Dar es Salaam, Bwana Peres Masige (wa pili kulia), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Bi. Adriana Lyamba na kulia ni binti wa mshindi huyo, Mary Mbasha. Promosheni hiyo iliyoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Letshego, mshindi alitakiwa kuweka akiba kwa kutumia huduma ya Timiza inayopatikana kwa watumiaji wa Airtel Money
Ni furaha tu kwa mshindi wa promosheni ya 'Vimba na Timiza Ushinde' Bwana Peres Masige (kulia) akiwa na binti yake, Bi. Mary Mbasha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo ya bajaji na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Bi. Adriana Lyamba, jijini Dar es Saaam leo. Promosheni hiyo iliyoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Letshego, mshindi alitakiwa kuweka akiba kwa kutumia huduma ya Timiza inayopatikana kwa watumiaji wa Airtel Money
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Bi. Adriana Lyamba (kushoto), akikabidhi zawadi ya smart televisheni aina ya Samsung inch 50 kwa mmoja wa washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Upige Mwingi na Airtel' mkazi wa Dar es Salaam, Hussen Hussen, Katika hafla iliyofanyika jijini humo leo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Bi. Adriana Lyamba (kushoto0, akikabidhi zawadi ya jokofu kwa mshindi wa promosheni inayoendelea ya 'Upige Mwingi na Airtel' mkazi wa Dar es Salaam,Sabina Joseph, Katika hafla iliyofanyika jijini humo leo.

Post a Comment