Header Ads

test

SERIKALI YATOA BILIONI MOJA KUTEKELEZA MIRADI YA BOOST NA SWASH MADABA

Na Albano Midelo,Madaba

Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni moja kutekeleza miradi ya BOOST na SWASH katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Wakili Sajidu Mohamed amesema Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi milioni 610 kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule
sita za msingi.

Wakili Mohamed amebainisha zaidi kuwa Halmashauri hiyo pia imepokea zaidi ya shilingi milioni 436 kupitia mradi wa SWASH kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji katika shule za msingi 11 .

Ameitaja miundombinu mingine inayotekelezwa kupitia mradi wa SWASH kuwa ni ujenzi wa kisima,ujenzi wa kichomea taka,ujenzi wa placenta na ujenzi wa sehemu ya kunawia mikono katika zahanati ya Gumbiro.

“Kwa niaba ya wananchi wa Madaba,tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuletea fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo’’,alisema Wakili Mohamed.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kusimamia kikamilifu miradi hiyo ili iweze kukamilika katika ubora na viwango ili iweze kuanza kutumika .

Serikali ya Awamu ya Sita imetoa zaidi ya shilingi bilioni 7.7 kutekeleza mradi ya uboreshaji miundombinu ya elimu katika shule za msingi (BOOST) mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya BOOST na SWASH katika  Halmashauri ya Madaba wilayani Songea


Baadhi ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa kupitia mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi BOOST katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea

No comments