MJUMBE JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA SINGIDA ASHAURI WANANCHI WACHUKUE TAHADHARI YA MVUA
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida Ahmed Misanga amewaomba wananchi kuchukua tahadhari mapema ya tahadhari ya mvua kubwa kupita kiwango cha Elnino kwa kuhakikisha njia za maji zinakuwa safi na hakuna uchafu wa kuzuia maji kupita.
Kwa mujibu wa tahadhari ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania( TMA) ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kunyesha mvua kubwa kuanzia Oktoba mwaka huu.
Akizungumza leo Misanga amesisitiza kutokana na tahadhari ya TMA ni vema wananchi wakaanza kuchukua hatua ikiwemo kusafisha mitaro na njia za maji kama hatua kupunguza madhara ya mvua hizo iwapo zitanyesha.
"Lazima kuchukuwa tahadhari mapema kwa kuhakikisha njia za maji ni safi na hakuna uchafu unao zuia maji kupita.Tusafishe mitaro ya maji na kuchoma taka zote na kama kuna majani ama miti katika mitaro ya maji yaondolewe yote
"Tuhahikikishe taka zote zinapelekwa katika dampo za taka ya miji yetu.Madampu yaliyopo katika makazi ,soko , mjini taka zisikae kwa muda mrefu, ziwe zinatolewa haraka na kupelekwa dampu kuu ili kuepuka magonjwa ya mlipuko...
"Kama magonjwa ya kuhara, kichocho na magonjwa mengine.Mvua zitakapo anza kunyesha na kuozesha taka katika makazi ya watu na maeneo yanayo wazunguka ndo huchochea magonjwa ya mlipuko, " amesema.
Post a Comment