Header Ads

test

RC SHIGELA AWAASA WADAU KUIGA HATUA ZA GGML.

 NA Nasra Ismail, Geita

Mkuuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela amewaomba wadau wengine waige mfano wa GGML katika kuwekeza na kufanya maendeleo katika jamii hasa katika sekta ya michezo.

Akizungumza mbele ya hadhara iliyojitokeza katika shughuli za kukabidhi basi LA kisasa lenye jumla ya viti 45 lenye thamani ya takribani sh mil 500  Shigela aliwashukuru GGML kwa namna inavyojitoa na kushirikiana na jamii.

Nae mkurugenzi mkuu wa GGML  Terry Strong alisema anafuraha kubwa kutangaza mchango huo wa basi jipya kabisa lenye viti 45 kutoka GGML kwa Geita Gold Fc.

Aidha bwana strong aliongeza kuwa GGML itaendelea kushirikiana na kilabu hicho ili kukuza vipaji vya vijana na kujenga maisha bora ya baadae kwa vijana.

Kwa upande wake mbunge wa Geita mjini Constantine Kanyasu aliwaombaa wachezaji wa Geita Gold kufanya vizuri uwanjani ili kuwatia moyo mashabiki kwani wanaumia pale inapofanya vibaya.

"Wananchi wa Geita wanawaamini sana na wanaipenda timu hii mnapokuwa uwanjani mjue mauvivu tunayoyapata huku yanapotokea mambo ambayo hatukuyatarajia tunayafanya haya kwasababu tunataka kupeleka furaha kwa wananchi wa Geita." Alisema Kanyasu.
 
Nae mtendaji mkuu wa Geita Gold fc Simon Shija alisema kuwa timu inakabiriwa na changamoto ya uwanja ambapo uwanja mpya wa Magogo bado haujakamilika hivyo inawalazimu kutumia uwanjani wa Nyankumbu Girls hali inayopelekea timu kukosa uwanja wa akiba na mazoezi.

Aidha aliongeza kuwa bado klabu inahitaji ongezeko LA wadhamini ili kuleta tija katika uendeshaji wa timu hiyo ambayo inaendelea kufanya vizuri katika ligi mbalimbali hapa nchini.

Pia timu imefanikiwa kutoa mchezaji anayewania tuzo ya goli bora la msimu  2022/2023 Elias Mruguu Maguri pamoja na kutoa mchezaji anayewania  tuzo za TFF za Mchezaji chipukizi ambaye ni Edmund G.John.

Shija aliongeza kuwa timu imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya ligi kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa msimu wa 2022/2023.

Kwa upande mwingine timu imefanikiwa kupata mdhamini mpya ambaye ni GF TRUCKS and EQUIPMENT pamoja na kufanikiwa kupata mdhamini wa mmiliki wa klabu halmashauri ya mji-Geita ambao ni kiasi cha sh 500,000,000.

"Timu kwa michezo ya nje imeweza kushinda mechi 5 za ugenini ikiwemo timu kutoka Sudan ya Hilal All Sahil FC ya Sudan katikabuwanja wa Chamazi Dar Es Salaam na KMC-Uhuru Dar es Salaam".Alisema Shija.




No comments