Header Ads

test

TEFA:HATUKO TAYARI KUFANYA UCHAGUZI KWA MAELEKEZO, TUNAIOMBA TAKUKURU ICHUNGUZE

 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

CHAMA cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke(TEFA) jijini Dar es Salaam kimeiomba TAKUKUTU na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuingilia kati sakata la mmoja wa viongozi wa soka walioko juu(jina tunalo) kulazimisha chama hicho kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti kinyume na utaratibu.

Kwa mujibu wa chama hicho baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wao kufariki dunia waliamua kufuata Katiba ya TEFA kwa kumchagua Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti kushika nafasi ya Mwenyekiti katika kipindi cha mpito wakati wakijiandaa kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka 2024.

Wamesema huyo anayelazimisha wafanye uchaguzi akiendelea viongozi na wajumbe wote wa TEFA katika wilaya hiyo wako tayari kuachana na chama hicho na kwenda kujiunga kwenye mchezo wa ngumi badala ya kubakia TEFA.

Akizungumza leo Oktoba 12,2023 mbele ya waandishi wa habari,Katibu wa Vilabu vyote vya Michezo Wilaya ya Temeke Habib Mbezi amesema mpira umekuwa ukiingilizwa na viongozi wa juu ambao hawajulikani huku akifafanua walipokea barua Oktoba 5,2023 wakitakiwa kufanya kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa TEFA.

“Jambo ambalo kimsingi kwa mujibu wa Katiba yetu sisi katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa kawaida viongozi waliokuwepo madarakani Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti kwa mujibu wa Katiba yetu kupitia wajumbe wa vilabu tulimuidhinisha kwani muda uliobakia ni mchache kwa maana ya mwaka mmoja basi yeye aongoze kwa kipindi cha mpito mpaka uchaguzi mkuu mwaka 2024.

“Chakushangaza huyo kiongozi wa juu akatoa maagizo kuwaambiwa DRFA ufanyike uchaguzi TEFA, kwanza ametudharau wana Temeke lakini pia ameidharau Katiba ya TEFA ambayo sisi viongozi wote wa vilabu tuliipitisha na tuliipeleka kwa Msajii wa vyama kuisaini na kuikubali.

“Tunasikitika sana huyo mtu wa juu anatoa maagizo kuwaambia DRFA uchaguzi lazima ufanyike. tulishasema tumemkaimisha Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti kuwa Mwenyekiti halali kwa kipindi hiki cha mpito mpaka uchaguzi mkuu ujao mwakani.

“Sasa huyu mwenye mamlaka huko juu anayelazimisha, tunasema hivi kwanza hatuko tayari kukubali kusiginwa katiba yetu.Sisi tuko na tunaendesha chama chetu cha michezo kupitia sisi wajumbe kwa mujibu wa katiba yetu ya TEFA si vingenevo.

“Sisi sio watu ama sio chama kinachoongozwa na huyo mtu wa juu, sisi ni chama ambacho cha michezo kinachojitegemea wilaya ya Temeke. Tunashangaa huyo mtu wa juu katoa maagizo kuwatisha viongozi wetu kwa kusema yoyote atakayesema neno lolote basi yeye atampeleka kamati ya maadili kwa maana hiyo atafungiwa na faini kama ipo atatozwa, hii ni dhuluma kubwa,”amesema.

Mbezi ameongeza TEFA kupitia yeye Katibu wa vilabu vyote vya michezo Wilaya ya Temeke wanasema hawatafanya uchaguzi na wako tayari kwa pamoja kuachana na mambo ya mpira na wataenda kujiunga katika mchezo wa ngumi kama wataendelea kulazimishwa.

“Tunaiomba Serikali kupitia Waziri wa Michezo aliangalie suala hili lakini tunaomba TAKUKURU ichunguze hili lina unini ndani yake , mbona wanatufuatafuata siye Temeke kwani huko kwingine hakuna?

“Watu wa Temeke vilabu vya Temeke hatupendi kuburuzwa na akiendelea kulazimisha tutajitoa kwa kuandika barua kwa Wizara ya Michezo na kwa Mama Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kuendeleza michezo na anatushika mkono lakini tunashaangaa baadhi ya watu wanaotoa maagizo wanatuharibia, waache.”

Kwa upande wake mmoja ya wajumbe wa Vilabu vya michezo Temeke Haji Mgaya amesisitiza hawako tayari kufanya uchaguzi sasa hivi huku akifafanua TEFA iko kihalali na hata Katiba yao ibara ya 38 kifungu cha nne kinasema kama changamoto yoyote ikitokea kwa Mwenyekiti na akashindwa kuendelea basi Makamu mwenyekiti wa kwanza anachukua nafasi hiyo.

“Hiyo ni kwa mujibu wa Katiba yetu lakini kuna watu wanataka kuvunja katiba halali ambayo imetoa muongozo .Lakini tukirudi katika mchakato wakati unaanza DRFA walisema wamepokea maelekezo na wao waliruhusu uchaguzi na DRFA waliruhusu TEFA isimamie uchaguzi wao wenyewe.

“TEFA walifanya usaili wakachukua wagombea wote na kuwaingiza katika uchaguzi.Hata hivyo DRFA waliamua kusimamisha uchaguzi na kutaka wao ndio wasimamie, hiyo haikubaliki.DRFA wametoa mtu mmoja wa kugombea , hii nchi ya demokrasia hakuna mgombea mmoja.”

Wakati huo huo Ashura Abdallah ambaye pia ni mmoja wajumbe wa TEFA amesema ; "Tunasema TEFA Uchaguzi hatatuki, hatuko tayari kupelekwa kama mzoga, tunajielewa na tunajua tunachokifanya, kwa mtindo huu TEFA hatuko tayari kufanya uchaguzi na hakuna binadamu yoyote anayeweza kujifanya yeye Mungu. Hatuogopi chochote , mchezo wa mpira wa miguu unatuburudisha.”









No comments