WAZIRI NDUMBARO AWAKABIDHI TUZO ZA HAPA JB NA SARAPHINA
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zilizopo chini ya Wizara ikiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) na Bodi ya Filamu Tanzania kuhakikisha wanawasidia wasanii kufikia soko la ushindani wa kimataifa.
Maagizo hayo ameyatoa katika utoaji wa tuzo za Kimataifa (HAPAAWARDS) kwa Mkongwe wa maigizo Jacob Steven 'JB' na msanii wa Bongofleva Saraphina Michael 'phina' walizozipata nchini Marekani Oktoba mwaka huu.
Dkt. Ndumbaro amesema sekta ya sanaa inatakiwa kuongeza ushindani katika masoko, ubora na usambazaji.
"Naviagiza Basata, Cosota na bodi ya filamu kuhakikisha wasanii wanafanya ushindani katika soko la kimataifa, kwa sababu itasaidia kuongezeka kwa pato la chumi na kuongeza ajira kwa vijana."
Waziri amesema ubora wa kazi wa wasani na kujituma kwao itakuwa chachu ya kuonekena katika anga za kimataifa.
"Pongezi kwenu wasanii JB na Saraphina kwa kushinda tuzo nchini Marekani hi imeleta heshima katika taifa na kuitangaza sekta ya Sanaa nchini."
Waziri amefafanua moja ya mikakati mingeni ni kuboresha tuzo za muziki na filamu ziwe katika kiwango cha Kimataifa.
Kwa upande wake Msanii na mtayarishaji wa kazi za filamu Jacob Stephen JB amesema anashukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika tasnia ya Sanaa na kufungua fursa mbalimbali za kuitangaza Tanzania na Kazi za Sanaa Kimataifa kupitia filament ya 'The Royal Tour '.
Jb pia ameielekeza tuzo hiyo kwa msanii mwenzake Single Mtambalike 'Rich ' kama mtu alieweza kumshawishi kuingia kwenye tasnia ya filamu wakati anafanya kazi kibaigwa kuchoma mahindi.
"Tangu nianze kuigiza mwaka 1997 sijawahi kupata tuzo nje ya nchi, imenipa nguvu ya kuongeza bidii katika kazi zangu, pia nimshukuru mwigizaji mwenzangu, Single Mtambalike ambaye alikuwa mtu wa kwanza kunileta katika Sanaa na kutambua uwezo wangu.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Leo Oktoba 17,2023 Jijini Dar es Salaam amemkabidhi Tuzo Mwakilishi wa Mwanamuziki Saraphina Michael ( Phina) kutoka Hollywood and African Prestigious Awards (Hapawards) 2023 ya nchini Marekani katika Kipengele Cha Mwanamuziki Bora wa Kike Muziki wa Bongo Fleva, Afrika Mashariki (Best Female in Bongo Fleva East Africa) zilizofanyika hivi karibuni nchini Marekani.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Leo Oktoba 17,2023 Jijini Dar es Salaam akimkabidhi Muigizaji wa Filamu Bw. Jacob Steven (JB) Tuzo ya Hollywood and African Prestigious Awards (Hapawards) 2023 kutoka nchini Marekani katika Kipengele Cha Muigizaji Bora wa Filamu "Best Bongo Movie Actor" zilizofanyika hivi karibuni nchini Marekani.
Post a Comment