NAMTUMBO WALIVYOBORESHA BWAWA LENYE RAMANI YA AFRIKA
Na Albano Midelo,Namtumbo
Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imeendelea kufungua milango ya
utalii kwa kuboresha vivutio vya utalii vinavyopatikana katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya amevitaja
miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyoendelea kuboreshwa kuwa ni
bwawa la Chengena lililopo kilometa sita kutoka mjini Namtumbo.
Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika kwenye bwawa hilo,Malenya
amesema bwawa hilo lenye umbo la ramani ya Afrika limeboreshwa na
kuchorwa majina ya nchi mbalimbali za Afrika na bendera zake.
“Mtu yeyote anaweza kuingia kwenye bwawa hili kwa kuingia kwenye boti
maalum na kufanya utalii wa ndani,akafika Chad,Algeria,South Afrika,
Kenya, Somaria na nchi mbalimbali ambazo zipo ndani ya
Afrika’’,alisisitiza DC Malenya.
Amesema wilaya ya Namtumbo imedhamiria kufikisha ujumbe kwa
watanzania kuwa hakuna haja ya Kwenda kwenye nchi hizo,wakati
unaweza kufika kwenye nchi hizo kupitia bwawa la Chengena Namtumbo.
Amesisitiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo itaendelea kutenga
fedha kwa ajili ya kuboresha vivutio mbalimbali vya utalii ili kuvutia watalii
wengi kutoka ndani ya Mkoa wa Ruvuma na nje ya Mkoa.
Hata hivyo amesema anawashukuru wadau mbalimbali waliotoa fedha za
kuanza kuboresha bwawa la Chengena ambazo zimewezesha kununua
mitumbwi kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani kwenye bwawa hilo na
kuchora ramani za nchi za Afrika.
Wananchi wilayani Namtumbo walijitokeza kwa wingi kwenye kivutio hicho
na kushiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwemo kuvutana Kamba na soka
ambapo Kaimu Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Namtumbo Shaibu
Majiwa amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuboresha kivutio cha bwawa
la Chengena na kuhamasisha michezo.
Amesema bwawa hilo lilikuwepo tangu zamani,hata hivyo halikuonekana
kama kivutio cha utalii ambapo hivi sasa watalii wanapata fursa ya kufanya
utalii kwenye bwawa hilo.
Majua ametoa rai kwa wananchi wa Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma
kuhakikisha wanafika kwenye bwawa hilo kufanya utalii wa ndani.
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Namtumbo Ndugu Acheni Mwinsheshe
Maulid amesema wilaya hiyo imeamua kumuunga mkono Rais kwa
kuhamasisha utalii ambapo amesema wilaya hiyo ina vivutio mbalimbali
vya utalii vikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na kivutio cha eneo la
Luegu ambako alijificha Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl.Julius
Nyerere katika harakati za kudai uhuru mwaka 1955.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo
amefunga tamasha la MANTRA CUP lililoshirikisha timu nane kwenye
mchezo wa soka.
Ligi hiyo iliyofanyika kwenye kivutio cha utalii Chengena ilianza Oktoba 28
mwaka huu na fainali kufanyika Novemba 12,2023 ambapo mshindi wa
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya akifanya utalii wa ndani kwenye bwawa la Chengena mjini Namtumbo ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wananchi kufanya utalii.Baadhi ya wananchi wa mjini Namtumbo wakifanya utalii wa ndani katika bwawa la Chengena baada ya serikali kuboresha bwawa hilo na kuwa kivutio kwa wengi.
Post a Comment