Header Ads

test

WANAWAKE WAZIDI KUSOGEZEWA HUDUMA ZA KIFEDHA NA BRAC

 

Katika kuhakikisha wanaendelea kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi, Taasisi ya BRAC Tanzania Finance Limited (BTFL) limetanua wigo wake wa kihuduma kwa kuzindua matawi mawili mapya katika Mkoa wa Ruvuma.

Uzinduzi huo wa matawi ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya shirika hilo ya kufikisha huduma za fedha karibu kwa watu wanaoishi katika mazingira yasiyofikika kirahisi hususani wanawake. 

Matawi hayo yamezinduliwa katika Wilaya ya Tunduru na Madaba na kwa mwaka huu wamezindua jumla ya matawi mapya 13 ili kuendelea kupanua huduma zao wakiwa na lengo ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii zetu nchini.

BTFL, inatoa huduma za kifedha kupitia mikopo midogo midogo kwa wajasiriamali na wakulima hasa wanawake na kwa sasa ina jumla ya matawi 177 yanayopatikana katika wilaya Zaidi ya 80 nchini kote.Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba, Adv. Sajidu L. Mohamed (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la BRAC, tukio hilo lilishuhudiwa na Mh. Diwani wa Kata ya Lituta, Orasmo Pili (katikati), Meneja Mkuu wa BRAC Kanda ya Dodoma, Bi. Roda Hassan (Kushoto), Pamoja na wafanyakazi wa BRAC (nyuma) katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika ofisini hapo Madaba mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Sande Mtatiro akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la BRAC Tanzaia Finance Ltd wilayani humo, mkoani Ruvuma.

No comments