Mauaji ya Madereva wa Malori ,Congo na Zambia tishio-TAMSTOA
CHAMA Cha Wamiliki wa Malori nchini(TAMSTOA) kimesema matukio ya kuuawawa,kujeruhiwa pamoja na utekaji wa mara kwa mara wanayofanyiwa madereva wa malori katika nchi za Congo na Zambia yamekuwa tishio kwa biashara usafirishaji wa mizigo kwakuwa yanasababisha hasara kubwa.
Akizungumza katika mkutano wa nne wa mwaka wa TAMSTOA,Mwenyekiti wa chama hicho Chuki Shaban amesema suala la usalama wa mizigo na madereva katika nchi za Congo na Zambia limekuwa tishio katika utekelezaji wa biashara ya usafirishaji mizigo.
“Hali hii imepelekea kuwa na matukio ya mara kwa mara ya utekaji wa magari ya mizigo inayosababisha hasara kwa wamiliki na madhara kwa madereva,mfano kujeruhiwa na wengine kuuawa kwa upande wa Congo na Zambia,”amesema Shabani.
Amesema kwakuona hilo Balozi za nchi husika zilitoa pendekezo kwa chama kutafuta wawakilishi katika nchi hizo ili kusaidia zoezi laufuatiliaji pale zinapoibiwa na madhara mengine yanapotokea.
Amesema pamoja na hayo bado matukio ya utekaji yanaendelea hivyo kuhatarisha Maisha ya madereva na kusababisha hasara kwa wasafirishaji.
“Chama kinaomba kupitia serikali kusaidia kushughulikia changamoto hii kwakuongea na kwa wa nchi husika ili kuboresha usalama kwa wasafirishaji wanapokuwa kwenye nchi hizo,”amesema Shaban.
Mbali na changamoto hiyo pia kuna wametaja tatzio la uhaba wa maegesho ya magari kutoka Dar es Salaam mpaka Tunduma ambayo wanadai kuwa yamekuwa machache sana na yenye mashaarti magumu inayopeleka kufanya huduma hiyo kuwa ngumu.
“Mfano maegesho ya magari Mbezi eneo hili aliruhusu mtu kufanya shughuli yoyote ya matengenezo endapo kutatokea dharula yeyote ,maegesho Kibaha kwa sasa yapo lakini sio rasmi,hatuhusiwi kupaki kabisa bila taarifa yoyote na baada ya hapo hakuna maegesho mengine yoyote mpaka Tunduma,”amesema Shaban.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Barabara Andrew Magombana akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara amesema kutokana na sekta ya usafirishaji kuwa kubwa sana kwa sasa na kufanya kuwepo kwa ongezeko la mizigo kwa asilimia kubwa zaidi ,serikali imefanya jitihada ya kutoa vibali vya ujenzi wa ICDs katika maeneo tofauti tofauti ili kuwezesha kutoa makontena bandarini.
“Pamoja na hayo serikali imeendelea kufanya juhudi kubwa za kuweza kukamilisha bandari ya Kwala lengo kuipa nafasi bandari ya Dar es Salaam ili kuiwezesha kupokea shehena nyingine zinazotolewa na meli,”amesema.
Mwenyekiti wa Chana Cha Wamiliki wa Malori nchini(TAMSTOA)
Chuki Shaban akizungumza katika mkutano wa nne wa mwaka wa chama hicho.
Baadhi ya Picha pamoja katika mkutano wa wamiliki wa malori
Post a Comment