Header Ads

test

WANASAYANSI CHIPUKIZI WAKABIDHIWA TUZO, PROFESA MKENDA AKOSHWA NA BUNIFU ZAO

 

Na Mwandishi Wetu.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda amekabidhi tuzo za washindi wa Shindano la wanasayansi chipukizi linaloratibiwa na Shirika la Wanasayansi Chipukizi (YST) huku akifafanua  mawazo ya kibunifu yaliyoibuliwa na wanafunzi wa shule za sekondari nchini yanayonesha kuna hazina inayohitaji kutunzwa na kuendelezwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Profesa Mkenda wakati wa kutoa zawadi kwa washindi hao,  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Profesa Bruno Sunguya amesema kupitia shindano hilo kumeonesha uwepo wa bunifu za hali ya juu.

Amesema miongoni mwa kazi hizo za ugunduzi zipo za mfumo wa akili bandia (AI) ikiwemo za umwagiliaji kuzuia upotevu wa maji magonjwa  katika mimea ya mazao kuzuia uduma u wa mimea na njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha katika tuzo hizo, wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru iliyoko mkoani Mwanza waliibuka washindi  wa jumla wakiwa na mradi uliotafuta usafi wa maji ya kunywa kwa shule za sekondari.

Mada hiyo inatokana na kuwepo Kwa tatizo la magonjwa  ya mara  kwa mara ya tumbo, amiba  kwa wanafunzi wa shule za bweni , hivyo kuhitaji kujua kiwango cha usafi na usalama wake.

Pamoja na hayo amesema tuzo hizo kwa wanafunzi zinasaidia kuhamasisha masomo ya Sayansi  katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii na kuongeza ubunifu katika nyanja mbalimbali kwani ni eneo linaliweza kuonesha vipaji vyao.
"Bunifu zinazoibuliwa na wanafunzi hawa ni zile zinazoendelea kutoa suluhu kwa matatizo ya kila siku yanayoikabili jamii," amesema Profesa  Sunguya kwa niaba ya Profesa Mkenda na kuongeza kuwa mawazo ya kibunifu ya sayansi yanasaidia kujenga nchi kwa vizazi vijavyo.

Ameeleza kwamba maonesho hayo yanahamasisha masomo ya Sayansi mashuleni katika kuleta mabadiliko  nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya YST,Profesa Yunus Mgaya amesema wanafunzi wamekuwa na mawazo ya kisayansi yenye kuwajenga  Kwa siku zijazo.

" Ni mawazo yanayofungua fursa mbalimbali za kufikia uluhu za matatizo yaliyopo katika jamii,ambayo ya ajenga kizazi chenye kupata suluhu za kisayansi," amesisitiza.

Wakati huo huo Mfadhili wa wanafunzi wanaoshinda katika tuzo hizo kutoka Karimjee Foundation Vinoo Sumaiya amefafanua kupitia tuzo hizo tayari wanafunzi 41 walishapata udhamini wa kusoma elimu ya vyuo vya elimu ya juu.



 

No comments