Header Ads

test

MBUNGE NDUGULILE KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA SHIRIKA LA AFYA DUNIA ,RAIS DKT SAMIA ABARIKI.








Na Mwandishi wetu

SERIKALI ya Tanzania imemtambulisha Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile kuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ukanda wa Afrika.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Leo Mei 9,2024 katika hafla ya utambulisho huo iliyohudhuriwa na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba,Amesema kutambulishwa kwa Dkt. Ndugulile ni ishara ya kufungua milango ya kampeni kuelekea kuwania nafasi hiyo muhimu.

Amesema nafasi hiyo ambayo anagombea Dkt Ndugulile ni nafasi muhimu sana na inabeba maslahi mapana ya wananchi katika masuala mazima ya afya zao.

"Nakupongeza sana Dkt. Ndugulile kwa kuidhinishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwania nafasi hii

"Dkt. Ndugulile ni mtu ambaye namemfahamu kwa muda mrefu, ni mchapa kazi ambaye amebobea katika masuala ya afya, akihudumu katika nafasi mbalimbali Serikalini ikwemo Waziri wa Afya, na amefanya kazi na taasisi mbalimbali za kimataifa, hivyo ninaimani anafaa kuwa katika nafasi hiyo," amesisitiza waziri Makamba.

Amefafanua kuwa WHO kwa Kanda ya Afrika inasimamia nchi takribani 48, hivyo miongoni mwa mambo ambayo atayafanya endapo atachaguliwa na kupata nafasi hiyo ni pamoja na kuendeleza mabadiliko katika shirika.

Naye Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo amesema kwa mara ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kutoa mwakilishi wa kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.

"Mgombea wetu anauzoefu mkubwa katika masuala ya afya Duniani, hivyo hii ni nafasi sahihi kwa Dkt. Ndugulile kwenda kuonesha uzoefu wake na kuiwakulisha Tanzania vizuri endapo atachaguliwa " amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake mgombea wa nafasi hiyo Dkt Ndugulile ambaye amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumuamini na kumpa kibali na kukubari kumuunga mkono katika kuwania nafasi hiyo.

No comments