MARIAM ULEGA ACHANGIA MILIONI 3 KAMPENI KUSAIDIA BAISKELI MTOTO MWENYE ULEMAVU PWANI
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
MJUMBE wa Baraza Kuu UWT Taifa ambae pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega amechangia Sh.milioni 3 kwa kikundi cha Pwani Generation Queens (Mwanamke Sahihi Fete) ili kuunga mkono kampeni ya kumsaidia baiskeli mtoto mwenye ulemavu wa viungo.
Amewataka wanawake kuiga kwa vitendo yale mazuri yanayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kusisitiza wanayo kila sababu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais katika kuleta maendeleo ya Watanzania wote.
Kuhusu tuzo hizo amesema wanatoa kama sehemu ya kutambua jitihada za watu mbalimbali ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo.
Pia amesema wameanzisha kampeni ya KOMBOA WATOTO WENYE ULEMAVU ambapo lengo lao kupata baiskeli 100 lakini hadi sasa wameshatoa 26.
Post a Comment