SINGIDA MJINI – AHMED MISANGA AENDELEA KUSAKA KURA ZA USHINDI KWA WAGOMBEA WA CCM
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida, Ndg. Ahmed Misanga, ameendelea na harakati za kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Singida Mjini.
Misanga amekuwa akipita mtaa kwa mtaa na kijiwe kwa kijiwe akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani kupitia CCM.
Akizungumza na wananchi wa Singida Mjini, Misanga amesema:


“Ushindi wa CCM ni ushindi wa maendeleo. Ni jukumu letu kuhakikisha Mama Samia anaendelea kupewa nguvu ya kuongoza nchi, wabunge na madiwani wetu wapewe nafasi ya kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa Singida.”
Amesisitiza kuwa mshikamano, mshikikano na kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi ni nguzo kuu ya kuimarisha chama na kulinda maslahi ya wananchi.

Post a Comment