Header Ads

test

Benki ya Absa na The Runners Club Wazindua Mbio za Absa Dar City Marathon 202


Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na The Runners Club, wamezindua rasmi mbio za Absa Dar City Marathon 2026, zinazotarajiwa kufanyika Mei 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo linatarajiwa kuvutia zaidi ya washiriki 5,000 kutoka ndani na nje ya nchi, likilenga kuhamasisha mazoezi ya mwili, mshikamano wa kijamii pamoja na maisha yenye afya.

Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na makundi matatu ya mbio; kilomita 21.1 (Nusu Marathon), kilomita 10 na kilomita 5. Usajili tayari umefunguliwa kupitia majukwaa rasmi ya usajili, huku wakimbiaji wa viwango vyote, kuanzia wanariadha wakongwe, wapenda afya, hadi washiriki wa burudani, wakihimizwa kujiandikisha na kushiriki katika sherehe hii ya kipekee jijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga, alisema:

“Katika Absa, tunaamini katika kuleta athari chanya katika jamii tunazozihudumia. Absa Dar City Marathon siyo tu mbio, bali ni jukwaa linalokuza afya, umoja na ustawi wa jamii, tunajivunia kushirikiana na The Runners Club kuandaa tukio hili na tunawahimiza Watanzania wote kukuuenzi mtindo huu wa maisha wenye kujishughulisha kimwili.”

Naye Mratibu wa mbio hizo na Makamu wa Rais wa The Runners Club, Godphrey Mindu, aliongeza:

“Marathon hii inaakisi ukuaji mkubwa wa utamaduni wa kukimbia nchini Tanzania, tumeona jamii zikija pamoja kupitia mazoezi ya viungo, na tukio hili ni sherehe ya roho hiyo, tunatarajia kuwapokea wakimbiaji wa viwango vyote na kutoa uzoefu wa hali ya juu siku ya mashindano.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Donald, alisema:

“Matukio kama Absa Dar City Marathon yana mchango mkubwa katika kuvumbua na kukuza vipaji vya riadha huku yakihamasisha afya na nidhamu. Kama chama, tunaunga mkono kikamilifu juhudi zinazokuza mfumo wa riadha na kuhamasisha kizazi kijacho cha wakimbiaji.”

Wawakilishi kutoka vilabu mbalimbali vya kukimbia walisisitiza umuhimu wa tukio hilo kwa jamii. Johnson Mbunda “Balozi” kutoka Goba Roads Runners alisema kuwa marathon hiyo “siyo tu mbio, bali ni tukio linalowaunganisha wakimbiaji kutoka kote nchini kukutana, kuwasiliana na kujenga urafiki wa kudumu.” Mwanachama wa Kigamboni Runners alielezea mbio hizo kama “mkusanyiko wa kila mwaka unaotoa fursa ya kuungana tena na marafiki na familia, kukutana na watu wapya na kuiona Dar es Salaam kwa mtazamo wa kipekee.”

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wanachama wa vilabu mbalimbali ikiwemo Tabata Runners, TOT Runners, Absa Running Club, Salasala Runners na Kigamboni Runners, pamoja na wadhamini wa tukio hilo. Uwepo wao uliashiria kukua kwa utamaduni wa kukimbia na mshikamano mkubwa wa jamii unaoliunga mkono tukio hili.

Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga (kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za mwaka huu za Absa Dar City Marathon zinazotarajiwa kutimua vumbi jijini Dar es Salaam, Mei 17 mwaka huu. Katikati ni Makamu wa Rais wa The Runners Club, Bw. Godphrey Mindu, waratibu wa mbio hizo na kushoto ni Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Jesca Nassari, ambao ni mmoja wa wadhamini. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa tukio mbio hizo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga (wa tatu kutoka kushoto), na Meneja Matukio na Huduma za Jamii wa benki hiyo, Bi. Abigail Lukuvi (kushoto kwake), wakionesha fulana zitakazovaliwa na wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Absa Dar City Marathon katika hafla ya uzinduzi wa maandalizi ya mbio hizo, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa The Runners Club, Bw. Godphrey Mindu, waandaaji wa mbio hizo na baadhi ya wawakilishi wa kampuni wadhamini. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa Absa Dar City Marathon.

No comments