Header Ads

test

MSD YAJIVUNIA MAFANIKIO UPATIKANAJI DAWA,VIFAA TIBA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma

BOHARI ya Dawa(MSD) ambayo ni taasisi iliyoundwa kisheria mwaka 1993 ikifuatiwa na maboresho mbalimbali ya sheria ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ya msingi imeendelea kujivunia mafanikio yaliyopatikana katika utoaji huduma za afya nchini.

Akizungumza leo Aprili 24,2026 wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na MSD na kuhusisha Wahariri na waandishi wa habari Mfamasia kutoka kitlendi cha Mipango,Ufuatiliaji na Tathimini Lilian Magesa kutoka MSD ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa kumekuwepo na mafanikio katika kipindi cha miaka minne 2021/22 hadi mwaka 2024/25.

Amefafanua katika kipindi cha miaka minne mapato ya MSD yameongezeka kwa asilimia 103 kutoka Sh.Bilioni 315.12 hadi kufikia kiasi cha Sh.Bilioni 640,5 mwaka 2024/25.

Pia mafanikio mengine ni kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za afya ashiri kutoka asilimia 42 mwaka 2021/22
hadi kufika asilimia 73 Machi, 2026.

“Hali ya utimizaji wa mahitaji wa vituo vya kutolea huduma za afya umeendelea kuongezeka kutoka asilimia 4l hadi kufikia asilimia 77 katika kipindi cha miaka minne.”

Pia amesema mafanikio mengine ni kuongezeka kwa mizunguko ya usambazaji wa bidhaa za afya kwenda vituo vya kutolea
huduma za afya kutoka mizunguko minne kwenda mizunguko sita kwa mwaka huku ununuzi wa bidhaa za kuwezesha uzazi pingamizi ( CEmONO) umefikia asilimia 100 ya
MS.

Ameongeza kuwa mafanikio mengine mashine 162 za kusafisha damu(dialysis) zimesambazwa kutoka mashine 60 mwaka 2021/2022 zilizogharimu Sh.bilioni 10.14

Pia kukamilisha ujenzi wa maghala ya kisasa yanayokidhi viwango vya uhifadhi na kuanza kutumika katika Kanda ya Dodoma na Mtwara -mita za mraba 12,000.Aidha kuanza kwa ujenzi wa ghala la Chato mkoani Geita lilifikia asilimia 42 ya utekelezaji.

Mafanikio mengine ni uanzishwaji wa kampuni tanzu ijulikanayo kama MSD Medipharm Manufacturing Company yenye jukumu la kusimamia uzalishaji unaotekelezwa kibiqshara na kwa ufanisi mkubwa .

“Pia kiwanda cha mipira ya mikono -Idofi kukamilika na kuanza kazi rasmi ya uzalishaji Februari 2024 pamoja na ongezeko la thamani ya bidhaa zinazonunuliwa kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutoka Sh.bilioni 15.90 zilizonunuliwa mwaka 2021/22 hadi Sh.bilioni 98.72 mwaka 20/2024/25.”

Kuhusu changamoto amesema mojawapo ni uhaba wa mtaji wa kuwezesha;Ununuzi wa bidhaa za Afya toshelevu kwa kiwango cha miezi 5, Ujenzi wa miundombinu toshelezi na inayokidhi viwango vya uhifadhi pamoja na ushiriki na uanzishai wa viwanda vya bidhaa za afya.

Pia uwepo wa madeni, Washitiri kuchelewa kuleta bidhaa za afya kulingana na mikataba,ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia bidhaa za Afya licha ya kuongezeka kwa idadi ya watu na mahitail na utegemezi wa uagizaji kutoka nje ya nchi kutokana na uwezo hafifu wa viwanda vya ndani.








No comments