Header Ads

test

TEN/MET YACHANGIA MIL 53.2 KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU SONGWE

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akizungumza wakati akifunga rasmi Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026 yaliofanyika Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro akihutubia wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, yaliofanyika kwenye Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu waliofanya vizuri kwenye somo analofundisha katika Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026 yaliofanyika Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akihutubia wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, yaliofanyika kwenye Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Sehemu ya wadau wa elimu wakiwa kwenye hafla ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, yaliofanyika katika Halmashauri ya Momba, Mkoani Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akipokelewa alipowasili kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.


Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akitembelea mabanda mbalimbali ya wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akitembelea mabanda mbalimbali ya wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akitembelea mabanda mbalimbali ya wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye (mwenye skafu) akiteta jambo na Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala (wa pili kushoto) kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro akifuatilia.
Sehemu ya wanafunzi na wadau wa elimu wakiwa kwenye maandamano ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, yaliofanyika katika Halmashauri ya Momba, Mkoani Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye (mwenye skafu), Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro (wa pili kulia) na Mratibu wa TEN/MET, Bi. Martha Makala (wa kwanza kushoto) pamoja na meza kuu wakipokea maandamano ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akwa katika picha ya pamoja na wadau wa elimu  kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.

Na Mwandishi Wetu, Songwe

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umechangia kiasi cha shilingi Millioni 53,250,000 ikiwa ni mchango kutatua baadhi ya changamoto za elimu zilizobainika kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Elimu Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.

Akizungumza katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya Juma la Elimu Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Bw. Simon Nanyaro alisema fedha hiyo imetoa kusaidia kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwenye baadhi ya shule zenyechangamoto.

Akifafanua zaidi, Bw. Nanyaro alisema shilingi milioni 26,000,000/= zitatumika kukamilisha ujenzi wa boma la madarasa mawili na ofisi moja ya walimu katika Shule ya Msingi maalum ya Ndalambo pamoja na kugharamia viti mwendo vitatu kwa wanafunzi wenye ulemavu shuleni hapo vyenye thamani ya shilini million 2,250,000/=.

Alisema shilingi milioni 5,000,000/= zitatumika kugharamia utengenezaji madawati 60 kwa Shule ya Msingi Msia, huku shilingi milioni 20,000,000/= itumike kukamilisha ujenzi wa darasa moja kwenye shule ya Msingi Chiwanda.

“…TEN/MET tunapenda kupongeza jitihada za Serikali katika kutoa fursa ya elimu kwa wote, kwa mfano Mpango wa Elimu Changamani (IPOSA) ambayo kwa mkoa huu ina jumla ya washiriki 1,256. Lakini pia MEMKWA yenye jumla ya washiriki 2,922 na jambo zuri zaidi ni Elimu Masafa ambayo kwa mkoa huu tumetaarifiwa kuwa ina jumla ya washiriki 23,” alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi ya TEN/MET.

Aidha alisema miongoni mwa changamoto walizozibaini kipindi chote cha maadhimisho ni pamoja na wanafunzi kutembea Umbali Mrefu kufika shuleni, upungufu wa miundombinu ya kujifunzia kama madarasa, matundu ya vyoo, maabara, maktaba na vifaa vya amali. Ukosefu wa Karakana kwa shule ya sekondari  Msangano inayotoa masomo ya Amali, kutokuwepo kwa vifaa wezeshi vya kujifunzia kwa vitendo kwa fani ya afya ya Wanyama (animal health production) - shule ya sekondari ya amali Msangano na uhaba wa madawati kwa baadhi ya shule za msingi na sekondari.

Kwa upande wake Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akizungumza wakati akifunga rasmi Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, ameupongeza Mtandao wa Elimu Tanzania kwa kuratibu kwa mafanikio makubwa maadhimisho hayo, pamoja na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

“GAWE 2026 imekuja katika wakati muhimu sana ambapo sekta ya elimu inahitaji mjadala wa kina kuhusu uendelevu wa ufadhili wa elimu. Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeshuhudia kupungua kwa misaada ya maendeleo katika sekta ya elimu, hali ambayo inaathiri uwezo wa nchi nyingi kuendelea kuboresha ubora, usawa, na ujumuishaji katika elimu,” alisisitiza Dkt. Simbeye.

Pamoja na hayo, Dkt. Simbeye ametoa wito kwa wadau wote wa elimu kuhakikisha  wanaimarisha usimamizi na uwajibikaji wa wazazi na jamii kushiriki kikamilifu katika elimu ya watoto kwa kuhakikisha wanawaandikisha na kuwasimamia kukamilisha mzunguko wao wa masomo, huku akiitaka Sekta binafsi kuwekeza zaidi katika elimu, na asasi za kiraia kuendelea kuhamasisha mabadiliko ya kijamii.

Kauli mbiu ya GAWE 2026 inahimiza “Ugemaji Rasilimali za Ndani kwa Elimu Jumuishi, Bora na yenye Kuzingatia Mahitaji Maalum”. Yaani “Domestic Resource Mobilization for Equitable, Quality and Inclusive Education” ambayo imekuwa mwongozo muhimu wa mjadala na hatua katika maadhimisho haya.

Matukio anuai kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, yaliofanyika kwenye Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephreim Simbeye akitembelea mabanda mbalimbali ya wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.
Matukio anuai kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2026, yaliofanyika kwenye Halmashauri ya Momba, Mkoa wa Songwe.

No comments