Header Ads

test

WASHIRIKI JUMA LA ELIMU 2026 WATEMBELEA SHULE MBALIMBALI WILAYANI MOMBA

AVvXsEglNLJKY6LBgRkY40y-9IXeBP2wVZc4HKZU1qIWoEiNe28hwN0Xh6-EQXENFDDF21sFq5sZ9OB-Duvbi2MLT7Z4mwvfMr0uWIcL8XqIQ1zciUV9wwlB0gTGf5RnVz1EvoHOwgdyPbTy8aT04g57CW5FtSnCtC7BH8McBAy2IQL4CoATn85z-I05qkn8ABec/s1412/IMG_4204.jpg" imageanchor="1" style="margin-left: auto; margin-right: auto;">Wadau mbalimbali wa elimu wakiwa katika mikutano na Wanafunzi wa baadhi ya Shule za wilayani Momba, ambapo maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika.

MAADHIMISHO ya Juma la Elimu Kitaifa yanaendelea Mkoani Songwe ambapo TEN/MET na wadau wa Elimu nchini wametembelea shule ya wasichana ya Songwe, Wilayani Momba. Shule hiyo iliyoanza na wanafunzi 25 chini ya usimamizi wa mkoa, sasa imekua hadi kufikia idadi ya wanafunzi 161 na walimu 15 wenye dhamira thabiti ya kuinua elimu ya mtoto wa kike.

Akizungumza na wadau wa elimu, Mkuu wa Shule Bi. Janeth Mwamwile amesema kuwa kwa miaka minne mfululizo shule imepata ufaulu wa asilimia 100, na hivyo kung’ara katika ngazi ya wilaya, mkoa na hata taifa. Lakini pamoja na mafanikio hayo, amebainisha shule bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo za miundombinu kama nyumba za walimu, maabara, bwalo la chakula, mabweni, jengo la utawala, jiko hivyo kutoa wito kwa wadau wa sekta ya elimu kuwashika mkono ili kuchochea mafanikio hayo.

Kwa upande wa Mtandao wa Elimu Tanzania @tenmet Bi. Martha Makala, Mratibu wa Mtandao), amesisitiza umuhimu wa kusaidia wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao akitolea mfano wa Elimu yake aliyoipata kutoka shule ya wasichana kama chachu ya kufanikiwa maishani. Aidha, Bi. Makala ameahidi kuwa changamoto zilizobainishwa zimepokelewa na zitachakatwa ili kuona namna wadau wa TEN/MET wanavyoweza kushirikiana katika utatuzi wake.

No comments