Header Ads

test

AFYA YA MAZINGIRA NI MSINGI MUHIMU WA AFYA YA WANANCHI,USTAWI WA JAMII’

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira ()limesema linaamini kuwa afya ya mazingira ni msingi muhimu wa afya ya wananchi, ustawi wa jamii, usalama wa majengo na maendeleo ya uchumi wa Taifa. Hivyo, kuna umuhimu mkubwa wa Serikali, sekta binafsi, wataalamu, vyombo vya habari, wananchi na wadau wote kushirikiana kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa salama, safi na yenye kulinda uhai wa watu na rasilimali za Taifa.

Hayo yameelezwa na Boniventura Mwalongo

Ambaye ni Katibu Mkuu Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kuhusu afya ya mazingira ,madhara ya chemba kujaa au kuziba ambapo ametoa mwito hatua za haraka zichukuliwe.

“Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira linatoa tamko hili kwa umma kutokana na ziara ya Katibu Mkuu wa Shirika hilo katika eneo la Soko la Kimataifa Kariakoo, Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya baadhi ya wadau wa afya, mazingira na maendeleo ya jamii kuomba kufika na kujionea hali halisi ya mazingira yanayozunguka eneo hilo muhimu la biashara ambalo ni uso wa uchumi wa Taifa letu.

“Katika ziara hiyo, Shirika limebaini umuhimu mkubwa wa kuongeza usimamizi wa afya ya mazingira, mifumo ya maji taka, chemba, mifereji ya maji, usalama wa majengo na kinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu na shughuli za kiuchumi nchini,”amesema Mwalongo.

Ameongeza madhara ya chemba kujaa au kuziba husababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, homa ya matumbo, kuhara, magonjwa ya ngozi na maambukizi mbalimbali.Uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji kama mito, visima, mabwawa na bahari.

Pia kuongezeka  kwa harufu mbaya, wadudu na mazingira hatarishi kwa afya za wananchi,kuharibika kwa misingi ya majengo, miundombinu ya maji na mifumo ya umeme,kuongezeka kwa hatari za mafuriko, moto na majanga mengine ya mazingira pamoja na kuathiri shughuli za biashara, afya ya wafanyabiashara na taswira ya Taifa mbele ya wawekezaji na wageni.

Hata hivyo shirika hilo limetao  mwito jamii kuelimishwa kuhusu afya ya mazingira,kuibua changamoto zinazohatarisha afya za wananchi,

kuhamasisha uwajibikaji wa jamii na kusaidia Taifa kujenga utamaduni wa usafi, kinga na ulinzi ikwa mazingira

No comments