Header Ads

test

WATUMISHI WA NBAA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2026 DAR ES SALAAM


Watumishi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka 2026, yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Ilala, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mhe. Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ambaye alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kutambua nafasi yao katika kujenga taswira ya serikali. Alieleza kuwa mfanyakazi mmoja anaweza kuchangia serikali kupendwa au kuchukiwa, hivyo aliwahimiza wafanyakazi wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, weledi na kujituma, akibainisha kuwa serikali inawajali na kuthamini mchango wao.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yameambatana na kaulimbiu isemayo: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”

Ushiriki wa watumishi wa NBAA katika maadhimisho hayo unaonesha dhamira ya taasisi hiyo kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza utamaduni wa kazi, uwajibikaji na maendeleo endelevu nchini.
Baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakipita mbele ya Jukwaa kuu huku wakiwa na bango lenye ujumbe kuhusiana Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments