TRAMEPRO YATOA WITO WA MAZUNGUMZO YA DHARURA KUTATUA MGOGORO WA MADEREVA
TRAMEPRO imesema kusitishwa kwa baadhi ya huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kumeathiri shughuli za wananchi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Kilimanjaro.
Shirika hilo limeeleza kuwa sekta ya usafirishaji ni muhimu kwa uchumi na maisha ya wananchi, hivyo mgogoro ukiendelea unaweza kuathiri usafirishaji wa abiria, chakula, dawa, mafuta, mazao na bidhaa nyingine muhimu.
TRAMEPRO imeitaka , LATRA na mamlaka nyingine husika kuitisha kikao cha dharura, kusikiliza madai ya madereva na kuhakikisha hatua zinazochukuliwa zinafuata sheria na haki za pande zote.
Aidha, madereva wametakiwa kutumia njia za kisheria na za amani katika kuwasilisha madai yao, huku wamiliki wa mabasi na malori wakitakiwa kuheshimu haki, usalama na ustawi wa madereva.
TRAMEPRO imesisitiza kuwa haki ya dereva, mwajiri, abiria na mwananchi inapaswa kulindwa.
“Haki ya mmoja isiwe sababu ya kuvunja haki ya mwingine.”
Taarifa hiyo imetolewa na Boniventura Ferdinand Mwalongo, Katibu Mkuu wa TRAMEPRO.

Post a Comment