ALICHOZUNGUMZA KATIBU MKUU WA CCM BAADA YA KUTEMBELEA KIWANDA CHA MBOLEA BABATI,MANYARA
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Daniel Chongolo ametembelea mradi wa ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha ITRACOM kilichopo eneo la vilima vitatu wilaya ya babati vijijini mkoani manyara ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.
Chongolo akiwa kiwandani hapo amemtaka mwekezaji huyo ambae ametoka nchini Burundi kukamilisha mradi huo ili kusadia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kwa kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi.
Chongolo amesema wataendelea kufanya utafiti wa ubora wa mbolea hiyo japo taarifa za awali zinaonyesha mbolea hiyo ni bora na kuahidi kuongeza msukumo wa wakulima kutumia mbolea kutoka kiwanda cha ITRACOM.
Kwa upande wake Katibu wa NEC - Organaizesheni Issa Haji Ussi (Gavu) amesema mbolea ni pembejeo muhimu kwa mkulima katika kumuongezea mkulima kilimo chenye tija, hivyo kufunguliwa kwa kiwanda hicho kitasaidia kupuguza gharama za uzalishaji kwa mkulima.
Post a Comment