BARAZA LA CHUO MZUMBE LAANZA KAZI KWA KUTEMBELEA MIRADI
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, walioteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia, wamekutana kwa mara ya kwanza katika kikao cha maalumu cha 124,
kilichofanyika Kampasi Kuu Morogoro, Jumanne tarehe 28 Februari 2023, kikiongozwa na
Mwenyekiti Prof. Saida Yahya- Othman.
Akiwakaribisha katika kikao hicho, Prof. Saida ameeleza furaha yake ya kupata wajumbe wa
Baraza, na kuwaahidi ushirikiano katika kutekeleza malengo ya Baraza hilo katika kusimamia
utendaji wa Chuo, ambao utazingatia kanuni, taratibu, sheria na miongozo iliyopo katika
kuhakikisha Baraza linafanya kazi zake kwa weledi.
Amewaahidi ushirikiano katika kipindi chote cha uongozi wake, huku akiwataka kuwa huru
kkuchangia na kuleta mawazo mapya ambayo yatafanya Chuo kiweze kusonga mbele kitaaluma.
Akiwakaribisha wajumbe hao kwa niaba ya Menejimenti, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.
William Mwegoha, amewapongeza na kuwakaribisha wajumbe hao Chuo Kikuu Mzumbe, na
kueleza kwa undani shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Chuo hicho katika kutoa elimu,
Utafiti, Ushauri wa Kitaalamu na Huduma za Jamii, huku akiwahakikishia ushirikiano katika
kuhakikisha kwa pamoja Chuo Kikuu Mzumbe, kinapiga hatua kimaendeleo.
Pamoja na kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotekelezwa na chuo hicho eneo la Maekani yakiwemo mabweni ya wanafunzi na jengo la
madarasa lililokamilika, ujenzi wa eneo la mahafali na jengo jipya la utawala, pamoja na
kutembelea Kituo cha Afya na Jengo la Utawala.
Wajumbe wa Baraza walipowasili katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo na kupokelewa na
wenyeji wao, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha na Naibu wake
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.Mwegoha (kushoto), akiwaongoza Wajumbe wa Baraza
kutembelea hosteli za Maekani. Kulia kwake ni Mjumbewa Baraza, Bi. Suzane Ndomba.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.William Mwegoha, akiwaonesha Wajumbe wa Baraza
ramani ya eneo la ujenzi Maekani iliyotokana na na Mpango Bora wa Matumizi ya Ardhi
ulioidhinishwa na Baraza (Master Plan).
Wajumbe wa Baraza wakipokea maelezo kutoka kwa Prof. William Mwegoha (Mwenye Suti),
kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi Maekani.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe
Prof. Saida Yahya-Othman (katikati), baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha utambulisho
kilichofanyika Makao Makuu ya Chuo, Morogoro.
Post a Comment