Wakazi wa Kata ya Kinyerezi wakiwa upande wa pili wa Daraja la Majoka ambalo limekuwa likihamahama Sasa Daraja Hilo litajengwa kwa shilingi Million 600.
Na Humphrey shao Michuzi Tv
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki Amewatoa hofu wakazi wa Kata ya Kinyerezi na kusema ujenzi wa Daraja la majoka utakamilika Julai mwaka huu.
Waziri Kairuki Amesema hayo Leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo Hilo ambalo limekuwa na changamoto kwa muda mrefu
" Mmemsikia Mtu wa Tarura hapa ambaye Amesema Tenda inafunguliwa kesho hivyo kufikia mwishoni mwa mwezi julai ujenzi wa eneo hili utakuwa unekamilika" Amesema Waziri Kairuki.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa eneo Hilo kuwa walinzi wa miundombinu inayojengwa na Serikali hili iweze kuwasaidia wao kwa muda mrefu kuliko kufanya uharibifu nankurudi katika shida Tena.
Kwa upande wake Mhandisi na Meneja wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geoffrey Mkinga Amesema wao kama Tarura washatembelea eneo Hilo zaidi ya mara tatu na tayari kesho tenda inafunguliwa
Mhandisi Mkinga Amesema ujenzi wa Daraja Hilo utagharimu zaidi ya Milioni 600 za kitanzania.
Nae Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli amemshukuru Waziri Kairuki kwa kutembelea eneo Hilo nakutaja kuwa Daraja Hilo ni kiunganishi kikubwa Cha wakazi wa Kinyerezi.
Aidha aliendelea kumshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya Maendeleo ya watu wa Jimbo la Segerea.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Angela Kairuki akizungumza na wakazi wa eneo la Kinyerezi Majoka
Post a Comment