Header Ads

test

BRELA: VIJANA UKIJISAJILI INAKUA RAHISI KUKOPESHEKA

 

Na Khadija Kalili

MSAJILI Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA) Yvonne Massele ametoa wito kwa vijana kote nchini kuchangamkia usajili kwani unawajengea uaminifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwarahisishia kupata fursa za mikopo katika Taasisi mbalimbali.

"Katika miaka ya hivi karibuni vijana wengi wamekuana mwamko wa kufanya biashara mbalimbali hivyo hatuna budi kutoa hamasa kwa vijana waweze kusajili Kampuni zao na jina la biashara kwa sababu usajili utawasaidia kutambulika kisheria katika biashara zao kitaifa na kimataifa.

Amesema hayo wakati wakitoa elimu ya Usajili wa Kampuni na majina ya Leseni ya biashara kwa wateja waliofika kwenye banda lao katika maonesho ya wajasiriamali na wafanyabiashara yaliyo fika tamati leo Februari 12 katika Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Massele amema kuwa BRELA hutoa huduma za Usajili wa Kampuni na Usajili wa jina la Kampuni pamoja na Hataza (Ubunifu wa aona yoyote ) hivyo amesema baada ya kuhitimishwa kwa maonesho haya waingie kwenye mtandao wajisajili wenyewe popote pale walipo kwa kufuata maelekezo.

"Kuna fursa ambazo mfanyabiashara anapata iwapo amesajili Kampuni yake
BRELA .

Aidha amezitaja fursa hizo ambazo zinapatikama endapo mtu akiwa amesajili BRELA kuwa ni pamoja na kupata tenda kubwa za kiserikali, unakuwa unatambulika kisheria lakini pia inaongeza sifa ya kupata Mikopo katika Taasisi mbalimbali za fedha.

Nicolous Masanja pamoja na Aisha Nasri wameshukuru Kwa elimu hiyo huku wakitoa wito na kuwataka watu wote kufanya hima kusajili Kampuni zao hata kama wana wazo ambalo ni muhimu ili kuwa na hatimiliki ya ubunifu wa biashara zao.

Kundi hilo la Vijana na wanawake limepata faida ya kufahamu misingi ya kuanzisha Kampuni kwa kusajiliwa kwani imebainika wengi wao wanafanya biashara zao bila kufanya usajili na hivyo inawanyima fursa ya kutambulika kisheria. Mteja akifurahia huduma za Usajili wa jina la iasha akiwa kwenye banda la BRELA
Kutoka Kushoto mteja aliyejitambulisha kwa jina la Nasri Abdi akipata maelezo namna ya kujisajili  kutoka kwa Afisa Tehama wa BRELA Fadhili Mlosa . 

No comments