Chadema yaghairi kuwahoji Mdee Bulaya na Matiko, sasa wajumbe wao saba kuhojiwa
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
Mawakili wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema , wameondoa mahakamani nia yao ya kuwahoji maswali ya dodoso Halima Mdee, Ester Bulaya na Ester Matiko juu ya kiapo kinzani walichowasilisha mahakamani hapo katika kesi waliyofungua kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho
Wabunge wengine katika kesi hiyo ni Wabunge hao ni Halima Mdee, Grace Tendega, Nursat Hanje, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Esther Matiko, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Felister Njau, Agnesta lambart, Asia Mohamed, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Styella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza na Naghenjwa Kaboyoka.
Hatua hiyo imefikiwa leo Machi 6, 2023 mbele ya Jaji Cyprian Mkeha wa Mahakama Kuu Masijala Kuu Dar es Salaam baada ya wakili wa Chadema, Hekima Mwasipo kuieleza mahakama kuwa wameamua kufunga maswali hayo baada ya kutafakari Kwa kina na kubaini kwamba hawana maswali ya ziada kwa wabunge hao.

Shauri hilo namba 36/2022 leo liliitwa mahakamani hapo kwa ajali ya Mbunge Jesca Kishoa kumalizia kuulizwa maswali ya dodoso na mawakili wa Chadema kuhusu malalamiko yake ya kufukuzwa uanachama kinyume Cha Sheria, lakini wakili Mwasipo akadai kuwa wamefunga kumuuliza maswali hayo.
Kishoa alianza kuulizwa maswali hayo ya Dodoso Novemba mwaka Jana huku akitanguliwa naTendega, Hanje, Pareso, Mwaifunga ambao walihojiwa maswali hayo ya dodoso kuhusu hati zao za viapo.
Baada ya kufunga maswali ya dodoso kwa Kishoa ndipo Mwasipo akaongeza kuwa, tulikwisha wasikiliza waleta maombi wengine na tulibakiwa na Mdee, Bulaya na Matiko kwa ajili ya kukamilisha zoezi zima la dodoso lakini baada ya kutafakari kwa kina na bodi ya wadhamini ya Chadema tumeona kwamba hatutakuwa na maswali ya ziada kwa hao waliobakia hivyo tunaomba kufunga tukio la maswali ya dodoso" amesema Mwasipo.
Kufuatia maombi hayo jopo la mawakili wa waleta maombi likiongozwa na Ipilinga Panya walidai kuwa hawana pingamizi juu ya maombi hayo
Baada ya kuwasilisha ombi Hilo, Jaji Mkeha alikubali ombi la kufunga maswali ya dodoso.
Aidha mahakama pia imekubali ombi la mawakili wa waleta maombi (Mdee na wenzake) la kutaka kuwahoji wajumbe saba wa bodi ya wadhamini Chadema juu ya kiapo kinzani walichowasilisha mahakamani baada ya kufunguliwa kwa kesi hiyo ya kupinga kuvuliwa uanachama kwa wabunge hao 19 wa viti maalamu Chadema.
Akiwasilisha ombi Hilo, Wakili Panya amewataja wajumbe wa bodi ambao ni, Dk. Azaveli lwaitama, Ruth Mollel, Mary Joackim, Francis Mushi, Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Hamis.
Jaji Mkeha alikubali ombi Hilo, kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 9,2023 ambapo wajumbe watakaoanza kuhojiwa ni Dk. Lwaitama na Mollel.
Katika kesi hiyo Mdee na wenzake wanawakilishwa na mawakili Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge na Edson Kilatu, ambapo Chadema wanawakilishwa na Kibatala, John Malya, Jeremiah Mtobesya na wengine watatu.
huku waliobaki wakiwa ni Esther Matiko, Esther Bulaya na Halima Mdee.
Wakati wabunge hao wanahojiwa na Kibatala walidai kuwa wao ni wanachama halali na wanakipenda chama hicho ndiyo maana walikisotea sana hadi kukaa mahabusu na pia walidai wao sio machizi kuwa wajipeleke Dodoma kuapishwa bila kupitishwa na chama chao.
Pia, walidai kuwa wanashangaa chama hicho kuwakana wao hadharani au kwa sababu wameshapata wengine ndiyo maana wamewatelekeza wao kwa madai kwamba hawakuchaguliwa.
Kesi hiyo namba 36/2022 lilifunguliwa Julai 22,2023 ma Mdee na wenzake wakiiomba mahakama itengue mchakato na uamuzi wao kuvuliwa uanachama ma Chadema na pia iwalazimishe kuwapa haki ya kuwasikiliza.
Pia, wanaomba amri ya zuio dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naTume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutokuchukua hatua yoyote hadi malalamiko yao yatakapotolewa uamuzi.
Pamoja na mambo mengine, wabunge hao wanadai kuwa mchakato na uamuzi wa kuwafukuza uanachama haukuzingatia matakwa ya kisheria na misingi ya haki, wakidai kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa.

Post a Comment