KAMATI YA KUDUMU YA MIUNDOMBINU YAIAGIZA TRC KUONGEZA KASI UJENZI WA RELI YA KISASA
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe, Seleman Kakoso
amemtaka Mkandarasi wa reli ya kisasa kwa kipande cha Dar es- salaam-Morogoro na
Makutopora kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yake ili aweze kukamilisha
mradi kwa wakati na muda uliopangwa.
Mhe, kakoso ameyasema hayo leo wakati kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu ilipokagua reli ya kisasa ya mwendokasi, kipande cha Dodoma-Makutupora na baadae Makutopora-Morogoro ikiwa ni utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
“Tunajua wakati mradi huu wa reli ya kisasa unaanza kulikuwa na changamoto nyingi na ndiyo kwanza miradi ya namna hii ilikuwa inaanza kutekelezwa nchini, lakini sasa Mkandarasi Yapi Merkezi ameshapata uzoefu wa kutosha na Serikali imemuongezea vipande vingine sasa ni jukumu lake kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yake ili huu mradi ukamilike haraka kwa mustakabali wa maendeleo ya sekta zingine na Taifa kwa ujumla kwani huu ni mradi wetu wa kimkakati kama Nchi,” amesisitiza Mhe Kakoso.
Akijibu maswali ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhe Atupele Mwakibete amesema Serikali ya awamu ya sita inaeendelea kuwekeza kwenye ujenzi na maboresho mbalimbali ya Miundombinu ya reli ya kisasa SGR na ile ya kawaida-MGR Nchini ili kuboresha Sekta ya Usafiri na Usafirishaji kwa njia ya reli katika kukuza uchumi.
“Serikali inafanya jitihada za kujenga na kuboresha sekta ya reli nchini na hata kujenga reli mpya za kisasa na kawaida kwa mikoa ambayo hapo awali haikuwa na reli kwa mfumo wa Public-Private partnership, ambapo mpaka sasa mazungumzo na wakandarasi yanaendelea ya ujenzi huo kwa maeneo ya Mtwara-Mbambabay itakayokuwa na urefu wa kilometa 1,000, Tanga –Arusha kilometer 1,028, na Dar es
salaam commuter network itakayokuwa na kilometa 1,600,” amesisitiza Mhe Mwakibete.
Awali akitoa salamu za ukaribisho Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bi Amina Lumuli ameishukuru kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa utekelezaji wa majukumu yake kwa shirika kwani imekuwa chachu kwa shirika kufanya vizuri na kuendelea kuimarika kiutendaji Bi Amina amesema utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa awamu mbalimbali umekumbwa na changamoto mbalimbali kama vile mlipuko wa uviko-19 ambapo baadhi
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi
Mhe Atupele Mwakibete akisisitiza jambo kwa Wakandarasi kutoka kampuni ya Yapi
Merkezi Wakati wa ziara ya kamati kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ya
kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha
2022/2023
Post a Comment