KILIO CHA WAKULIMA WILAYANI TUNDURU KUHUSIANA NA PEMBEJEO ZISIZO NA UBORA CHAPATA DAWA
Na Muhidin Amri, Tunduru
KILIO cha wakulima wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, kuuziwa pembejeo na viuatilifu visivyokuwa na ubora vilivyosababisha kushuka kwa uzalishaji na kushusha ari,kimefika mwisho wake baada ya Kampuni ya Bens Agro-Star Co Ltd kusambaza kwa wingi mbolea mpya ya asilia ya samadi ya Fomi.
Mbolea hiyo inayozalishwa hapa nchini,inatajwa ni mkombozi mkubwa wa wakulima kutokana na uwezo wa kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara ikiwamo zao maarufu la mpunga na mahindi yanayolimwa wilayani humo.
Akizungumza na wakulima wa kijiji cha Msinjili kata ya Mlingoni Magharibi wilayani humo katika shamba darasa ambalo limelimwa na kutumia mbolea ya Fomi,Meneja wa kampuni ya Bens AgroStar Ltd kanda ya Kusini Israel Mwampondele,amewataka wakulima kutumia mbolea hiyo ili waweze kuvuna mazao mengi kwenye msimu mmoja.
Amesema kuwa, kwa muda mrefu wakulima wanapoteza nguvu nyingi na muda mwingi kulima kilimo kisichokuwa na tija kwa kutofuata kanuni za kilimo bora na kutotumia mbolea za kupandia na kukuzia zinazofaa kwenye shughuli zao za kilimo.
Ameeleza kuwa,wananchi wengi wanapenda kulima,lakini changamoto kubwa bado hawazingatii taratibu na kanuni za kilimo bora,hivyo kupitia Kampuni ya Bens watahakikisha wanatoa elimu kwa wakulima kuhusu faida ya mbolea ya Fomi otesha na Fomi kukuzia.
Amesema,lengo la kampuni hiyo kuanza shughuli zake katika wilaya ya Tunduru na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla, ni kuwabadilisha wakulima kifikra kutoka kilimo cha mazoea hadi kufikia kulima kilimo cha kisasa na chenye tija na kutumia mbolea ya asili ya Fomi.
Dkt Mwampondele,amewataka wakulima mkoani Ruvuma kuanza kutumia mbolea ya Fomi ambayo kwa sasa ndiyo imekuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuzalishaji mazao mengi tofauti na ilivyo kuwa miaka ya nyuma.
Aliongeza kuwa,mkulima akitumia mbolea ya Fomi na kuzingatia kanuni na taratibu za kilimo chenye tija,faida yake ni kubwa kwani katika ekari moja ana uhakika wa kuvuna kati ya magunia 35 hadi 40.
Akielezea faida ya mbolea ya Fomi kwa wakulima wenzake Ramadhan Chalema aliyetumia mbolea hiyo kwenye zao la mahindi na mpunga alisema kuwa,hapo awali kabla hajaanza kutumia mbolea hiyo uzalishaji wa mazao ulikuwa mdogo ikilinganisha na sasa ambapo umeongezeka mara mbili zaidi.
Amewaomba wakulima wengine kuanza kutumia mbolea hiyo yenye uwezo mkubwa katika uzalishaji ili waweze kupiga hatua na hatimaye kujikwamua na umaskini kupitia shughuli zao za kilimo.
Afisa kilimo wa kata ya Sisi kwa sisi Lucy Komba alisema,wataendelea kushirikiana na kampuni ya Bens kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ya Fomi ili wakulima walime kilimo chenye tija na wapate faida kubwa kuliko sasa.
Aidha,amewashauri wakulima wilayani Tunduru kuanza kulima na mazao mengine kama mahindi,ufuta,alizeti na soya ambayo yanasoko la uhakika ili kujiongezea kipato,badala ya kulima zao moja tu la korosho ambalo kwa sasa linakabiliwa na changamoto kubwa katika uzalishaji na soko lake.

“nawaomba sana wakulima watutumie sisi wataalam wao ili waweze kulima kilimo chenye tija na waanze kutumia mbolea hiyo ya asili katika uzalishaji mashambani”alisema Komba.
Mkulima wa zao la mpunga wa kijiji cha Msinjili kata ya Mlingoti Magharibi wilayani Tunduru Ramadhan Chalema kulia akieleza faida ya kutumia mbolea ya asili katika kilimo cha zao hilo,kushoto meneja wa kampuni ya Bens AgroStar Ltd inayosambaza na kuuza mbolea ya asili ya Fomi,katikati afisa kilimo wa kata ya Sisi kwa sisi Lucy Komba.
Mkulima wa Nyanya chungu katika kijiji cha Msinjili Halmashauri ya wilaya Tunduru Abdala Mbako aliyeinama,akimuonyesha meneja wa kampuni ya Bens Agrostar Ltd inayosambaza na kuuza mbolea ya asili ya Fomi Dkt Israel Mwampondele nyanyachungu zilizowekwa mbolea ya Fomi. kulia afisa kilimo wa kata ya Sisi kwa sisi Lucy Komba.
Post a Comment