MAKAMU WA RAIS MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL FAISAL
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip
Mpango leo tarehe 08 Machi 2023 amekutana na kufanya mazungumzo
na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Al Faisal (Al Faisal Holding )
Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani Mazungumzo yaliofanyika katika Mji
wa Doha nchini Qatar.
Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais amemkaribisha mwekezaji
huyo nchini Tanzania kuwekeza katika fursa mbalimbali za kiuchumi
zilizopo ikiwemo katika miundombinu ya utalii kama vile Hoteli. Pia
Makamu wa Rais amesema Tanzania inayo fursa katika uwekezaji wa
viwanda vya dawa , kilimo pamoja na madini.
Kutokana na serikali kuhamishia shughuli zake katika makao makuu ya
nchi mkoa wa Dodoma, Makamu wa Rais amesema mkoa huo unayo
fursa ya kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za makazi, hospitali pamoja
na hoteli.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kampuni Tanzu ya Al Faisal (Al Faisal
Holding) Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani ameahidi kufanya ziara nchini
Tanzania pamoja na ujumbe wake ili kushiriki majadiliano ya pamoja
katika kuangazia maeneo muhimu ya uwekezaji ikiwemo elimu, afya na
uongezaji thamani ya mazao ya kilimo.
Ameongeza kwamba Tanzania imejaaliwa kuwa na fursa nyingi za
uwekezaji na kuahidi kuendelea kuwaalika wawekezaji wengine kutoka
katika baraza la ushirikiano la ghuba (Gulf Cooperation Council)
linalojumuisha nchi ya Qatar na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu.
Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani ni mwenyekiti wa kampuni tanzu ya Al
Faisal ilioanzishwa mwaka 1964 inajishughulisha na biashara mbalimbali
ikiwemo umiliki wa hoteli kubwa zaidi 20 duniani kote, makumbusho ya
kiutamaduni nchini Qatar, utengenezaji na usambaji dawa pamoja na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Al Faisal (Al Faisal Holding ) Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani Mazungumzo yaliofanyika katika Mji wa Doha nchini Qatar leo tarehe 08Machi 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Al Faisal (Al Faisal Holding ) Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani mara baada ya Mazungumzo yao yaliofanyika katika Mji wa Doha nchini Qatar leo tarehe 08 Machi 2023. (wengine ni Balozi wa Tanzania nchini Qatar Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk)
Post a Comment